Popular Posts

Thursday, December 5, 2019

ZIJUE SABABU ZA UGUMU UNAOPITIA 2⃣


By Elikado Mwasenga

➡ Fuatana nami katika kujifunza neno la Mungu lanye uzimA

➡ Ntaka nkuletee mwendelezo wa somo tulilokuwa nalo

 
 
➡ ```Nlikupa sababu ya kwanza inayolenga mfumo wa taarifa unazozipa nafasi ndani mwako```

Na tukaona ya kuwa kwa kiwango kikubwa Sana vitu unavyovipa nafasi kusikilza kutazama nk nk maadam tu vna uhusiano na kuingiza taarfa ndan yako na kutengeneza mfumo wa kimaamuz(Fikra)

Vina uwezo wa either kukupa hatua Bora zaid au kukurudsha nyuma

Leo nakupa sababu ingine inaweza kuwa sababu ya ugumu unapitia watu wengine wanaita jarbu

Nataka tusome maandiko kidgo

📖 Warumi:3.23
kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; 
Warumi:3.24
wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; 
Warumi:3.25
ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho

Yatazame kwa Makin maandiko haya

Anasema dhambi ilipoingia kwenye mfumo wa maisha ya mtu kilichofuata na *kuondolewa kwa utukufu wa Mungu juu yao*

Maana yake nn utendaji kaz wa Roho wa Mungu haupo juu yao tena

Na maandiko yako waz ya kwamba alipo Roho wa Mungu ndipo penye uhuru

Anhaa maana yake ni kwamba kuondolewa kwa utukufu(mazngra sahh kwa Roho wa Mungu kutenda kaz ndan na juu yako/yangu) kunaondoa na Uhuru

Na kuondoka kwa Uhuru kunazaa  kitu kingine kinachoitwa jaribu/teso/gumu unaloanza kulipitia

Ukisoma msatari wa mbele kidgo utaona kwa huruma zake Mungu akaondoa hilo teso kwa neema yake kwa kunuweka Yesu awe upatanisho wa sisi na Mungu yaani kuurejesha utukufu wake

Swali langu linakuja kwako kwanini pamoja na kwamba tumehesabiwa haki kwa neema still tunakuna na magumu kwenye maisha yetu,,,,

Naomba uelewe vzur juu ya hili eneo anapozungumzia kuhesabiwa haki kwa neema

📖 Fungua namimi kitabu cha mathayo 6

Matayo:6.12
Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. 
Matayo:6.13
Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.] 
Matayo:6.14
Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.

Ukisoma kwa makini maandiko haya na kutazama kile alichokisema kwenye warumi unaweza usielewe kidgo

Ngoja nkupe ufunuo wa ajabu kidgo

Kwanini nianze kuhangaika kuomba tena msamaha kwa Mungu na huku ninajua nimehesabiwa haki kwa neema

Yaaani kila kosa limefutwa kila laana haipo tena sasa kwanini niombe tena msaha??
➡ Kwanini

Mfano wewe mwanafunzi siku mkuu wako wa shule alipotangaza kila atakayepata " A" ya hisabati(mathematics) atampa zawadi alianza tu kugawa zawadi hata hamjaanza kufanya mtihani au alisubr mfanye mtihani aone matokeo ndipo agawe zawadi Sambamba na matokeo??

➡ Jibu unalo bila shaka

Pamoja na kwamba umeokoka umempa Yesu maisha yako hilo n Jambo moja kuna hatua ya ziada inahitajika

sijui kama unanielewa nnachotaka ukione hapa

haki tuliyohesabiwa hapa si kwamba haituhitaji tuombe toba mbele za Mungu hapana

Ni haki inayotupa uwezo wa kupokea msamaha kwa neema yaani tunasamehewa juu ya makosa tunayotubia japo kikawaida yalikuwa n makosa ambayo hata tungeomba msamaha tusingepata kusamehewa
➡ Hallelujah!

Kwa maana hiyo basi kuna watu tumo ndan ya yesu ila bado hatujajipatanisha naye kwa kiwango cha Yale magumu tunayokutana nayo kuondolewa

Sikia
 Anasema hivi basi msali hivi,,,,

➡ Mstari wa13 anasema usitutie majarbuni(kwenye magumu)

➡Tafakari kwa kina hapa

Unataka kuniambia Mungu hajui kama sisi tumo ndan yake tunamuamini kwanini tena tumuombe atuepushe na majaribu na huku anajua hatutaki kujaribiwa??

Na kwa bahati mbaya Sana waamini wengi hawana tabia ya kuomba ombi hili la Mungu kuwaepusha na majaribu matokeo yake n kwamba wanajikuta wanajarbiwa na kuajarbiwa

Maisha yao ni Vita Vita magumu kila leo

 Ukirsto wa namna hiyo mimi sioni raha yake hata kidgo

Mungu anataka tuEnjoy kuwa nayeye

Kwa hiyo sababu ingine inayopelekea kupitia ugumu unapitia n kwa sababu unakomaa Sana na hali yako

Wala sio mpango wa Mungu eti ukomae na hali yako kabisa sio mpango wa Mungu

Unasema kwa sababu gani unasema hivyo

Fungua na Mimi maandiko haya!

📖 Matayo:11.28
 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha .

Anataka umpe yeye masumbuko(magumu) yako mizigo yako ili upate pumnziko

Unajikuta unaanguka mara kwa mara kwenye zinaa

Unashia tu kusema leo ndo ilikuwa mwisho unajuta kabisa lakin siku mbili mingi usharud pale pale tena

Usipambane kwa nguvu zako nakwambia hutachomoka

Unapanga biashara yako unatafuta mtaji ukiaanza tu biashara hiyo haiana soko tena

Wala mbinu 12 za kuwa tajir ulizoziona YouTube hazitosh kukutoa hapo kuna nguvu ya ziada ya kiroho unahitaji

Kwa Nini umtwike yeye masumbuko na mizigo yako jibu hili hapa

📖 1 Petro:5.7
 ```huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.```


No comments: