Popular Posts

Monday, January 20, 2020

Nguvu ya wakati kwenye kusudi(Maono/Malengo)


Mhubiri:3.1
Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu .

Nataka nkutazamishe kwa ufupi juu ya namna ambavyo Muda Ni rasmali ya lazima Sana katika kufikia hatima au makusudio ambayo tumeyabeba kwenye maisha yetu ya kila siku

Kwa kawaida, kila binadamu hutamani kupiga hatua moja kwenda nyingine

Ingawa hii ni shauku ya kila mtu na ninaamini na wewe ni shauku yako pia lakini tujiulize kwa nini maisha ya watu wengi hayabadiliki?

Iweni kwenye uchumi iwe Ni kwenye Huduma yako au mahusiano yako na mwenza wake Angle yoyote ile kwenye maisha yako

Je unaona Kuna mabadiliko yeyote au Kuna namana umekuwa mtu wa shauku zisizo na matokeo yoyote kwenye maisha yako!??

Na huu ni mwanzo tu wa mwaka 2020 umeweka malengo gan wewe binafsi na mpaka Sasa katika mikakati ya kutimiliza malengo uliyonayo unajua upo kwenye hatua gan???

Pengine hata wewe unafuatilia somo hili una mawazo mengi sana makubwa ambayo yakifanikiwa  yatabadilisha maisha yako kwa kiwango kikubwa

Wakati tunauanza mwaka huu, karibu kila mtu alijiwekea malengo ya nini cha kufanya ndani ya mwaka kuelekea mabadiliko ya maana makubwa ya kushitua jamii aliyonayo

Mm cjui wewe umeweka malengo gani swali langu kwako lipo kwenye wakati wa kutimia kwa malengo yako

Haijalishi ukubwa au udogo umuhimu au lisilo muhimu lakn maandiko yanatueleza wazi kuwa Kuna majira(season) na wakati(time) _kwa kila kusudi_
Je upo kwenye season gan saiz ya malengo yako ??

Jambo la kujiuliza ni kwa nini watu wengi hawafanikiwi katika kutekeleza mawazo yao ?

Ulipanga mwaka huu lazima uwafikie watu 50 kwa injili ya Yesu ulipanga mwaka huu lazima uingize one million Jambo linalo niogopesha n kwamba sio mara yako ya kwanza kuweka mpango na bado hakuna mpango uliwahi kutimia mpaka leo hii

Umewahi kujiuliza Ni kwanini ?

Na shetan hamuogopi mtu anayeweka tu mipango na kuandika kwenye diary Kwan ni mara ngapi umeandika mawazo ya biashara mipango ya huduma umeona ushapiga hatua na bado hata haujaanza mwaka wa tatu sasa!

Shetan anaanza kupata shida tunapoaanza kupata ufahamu juu mambo madgo madgo yanayoweza kutusaidia kufikia hatima Bora

Na Jambo la kusikitisha n kwamba hayo mambo madgo madgo ndo yalee ambayo wengi wet tunayaona hayana uzito lakini kimsingi ndyo yaliyo beba uamuzi wa mwisho wa kipi tunaweza kufikia na kipi hatuwezi kukifikia

Mfano tabia za kawaida za kila siku huwa tunaona ni Jambo la kawaida kabisa lakn tabia ni eneo la ajabu Sana katika kutimiza malengo na mipango tuliyojiwekea

Naomba nkutazamishe kitu kidgo
Mpango wa Mungu kwa watu wake yaaani waamini n kuona wanamiliki na kutawala hapa duniani kwa ajili ya ufalme wa Mbinguni

Mimi sjui Kama unalitambua hilo
Na anaposema ninyi Ni Nuru ya ulimwengu chumvu ya dunia alikuwa na maana kubwa Sana sjui Kama umewahi kufikri uzito wa maneno haya

Mungu ametupa authority ya kubwa mno mno ila watu wenyewe Sasa walipewa authority ndiyo tatzo haswaa!

Nadhani unaelewa anaposema dunia na anaposema ulimwengu ni Kama anataka tuwe na mitazamo mikubwa achana na maono ya kutazama kuwa na influence kijijin pako tu hapo anataka uwe na picha kubwa

Kiasi cha kwamba maisha yako yanaweza yakaGovern ulimwengu wote kuliishia kusudi la Mungu
Unasema kivipi jiulize watu Kama akina Paulo akina Petro akina Keneth Hagin akina Martin Luther maisha yao n nuru halis ambayo mpaka leo inauwezo wa kuonyesha usahihi na ukosefu wa mambo mbali mbali katika ulimwengu woote

Kwann tunakuwa wazembe wazembe watoto wengi wa Mungu
Leo nataka nikupe Siri hiii
Yohana:8.32
 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru .

Maana yake Nini
Kumbuka uhuru(freedom) ni hali ya kufanya maamuzi bila ya kuingiliwa au kupingwa
Unakuwa na maamuzi binafsi

Moja ya kweli unazotakiwa kuzijua ni juu ya nidhamu ya Muda unapotaka kufikia ndoto yako
Sasa kinachokwamisha watu wengi Ni kwamba hatujui kuupangilia muda
Kwanini inakuwa hivyo?

Sababu chache Ni hizi

1.Hatuna vipaumbele
Mara chache Sana utaona watoto wa Mungu wanapangilia mambo yao ya kila siku 
Mfano hana jambo la ambalo asipolifanya kwa siku inampa shida ndani mwake badala yake Ni kwamba hata siku ikipita hajawaza au kutafuta maarifa Zaidi juu ya mipango aliyonayo katika maisha yake kwake anaona Kama Ni Jambo la kawaida 

Kimsingi tunatakiwa kuweka vitu kimkakati Yale mambo ya muhimu yanatakiwa yapewe uzito inapotokea inatakiwa kuamua juu ya kipi kifanyike kwa muda fulani unaamua kwa kutazam lipi Lina uzito 

2. Hatuna mambo maalumu tunayotaka kuyafikia 
Yaani hatuna maono na maisha yetu ya au hatima za maisha yetu matokeo yake Ni kwamba kila fursa inayokuja mbele yako kwako utaona inafaa

Hali hii imepelekea watu kutaka mafanikio ya haraka na wengi wanaishia kutapeliwa

Kuna mambo ukiyasikia utashaangaa Sana watu walivyotapeliwa hata ukielezewa unaweza ukajiuliza walimtapeli vipi eneo Kama hili mbona ako mzembe Sana si hvyo n kwamba watu tunataka tu chap chap upo juu hapana haiend hvyo Kuna mchakato  
3. Tunafikiri maisha Ni bahati tumesahau maandiko yanasema wakat wa bahati huwapa watu wote sio maisha ya bahati

Labda nikwambie tu kwamba maisha Ni mpangilio na mchakato Kuna hatua lazima uzipitie Kuna changamoto za kukutana nazo ambazo Ni lazima utafute namna ya kuzitatua mpaka kutikia hatima Kama unayasubr maisha ya bahati huenda mpaka tunakuzika ukawa mti yule yule wa toka unazaliwa 

4. Tunataka kufika bila kulipia GHARAMA ya tunayotaka kuyafikia

Watu wengi Ni wavivu hawataki kuomba wanataka upako hawawafanyi kazi wanataka kumiliki pesa ndefu 
Wanatumia pesa ovyo wanataka kumiliki magar ya GHARAMA 

hapana haiwezakani kwa sataili hiyo lazima ushughulike upambane 
Kuna sehemu maandiko yameandika neno gumu Sana 

Waebrania:12.4
Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi;

Fikiri juu ya hili eneo anasema kupambana kwenu na dhambi Ni zoezi linalohitaji pengine kupambana Kia's kwamba unaweza linganisha na kazi ya kukutoa damu!!!! Usitake usichofanyia kazi huo Ni uvivu na uzembe! 

MUNGU AKUBARIKI

No comments: