Popular Posts

Thursday, December 5, 2019

ZIJUE SABABU ZA UGUMU UNAOPITIA

Sehemu ya kwanza 1

By Elikado Mwasenga

BWANA YESU ASIFIWE SANA!!


Na kwanini ujue haya yote kwa sababu usichokijua ndicho kitakachokuangamiza

Kumbuka yasemavyo maandiko ya kwamba watu wake MungU huwa tunaangamia tunapokosa maarifa (tunapokuwa hatujui)

Kwa maana kwamba hatuangamii kwa SABABU Mungu hana nguvu hapana tunaangamia kwa sababu hatujui kama MungU Ana nguvu huwa tunasikia tuuy!

Kumbuka hili itakuwa n faida ya nafsi yako

Nataka tu uanze kwa kutambua kwamba kila jambo linaloendelea kwenye maisha yako lipo na sababu zake

Hata ugumu ulionao una sababu na tunavyoanza kutaka kutafuta suluhisho la tatzo tunaanza kutrace sababu zake Kwanza kutokea kwenye maisha yako

Fikiria umeanza kuumwa ghafla tumbo lako likawa kwenye maumivu makali
Ukakimbizwa hospital kutafuta solution ya shida yako

Jambo litakalokushangaza n kuona pamoja na kuwa maumivu hayo makali Jambo la kwanza daktari atakuuliza maswali Jana ulikula nn, imeanza saa ngap na Mambo kama hayo

Kwanini asikupe tu matibabu moja kwa moja

Anatafuta sababu!!

Ukiona mtu anasumbuliwa na nguvu za giza, anaombewa anapona anarud kule kule tena ujue Kuna sababu

Kuna sababu

Ukiona mtu anapambana kuutoa umaskn kwa bidiii zote, mtu anapambana kuacha zinaa, mtu Ana Pambana kufaulu masomo yake na bado anashindwa,,,, tambua hili Kuna sababu

MungU mwenyewe kiiila analolifanya Kuna sababu zake

Kila analofanya Kila analolipangilia huwa Lina sababu zake

inakuwa vigumu Sana kutoka hapo kwenda hatua Bora zaid kwa kuwa tu hautambui sababu ya ugumu unaoupitia

tafuta hata akiwa amefail Jambo lolote maishan wether ameanguka kibiashara mtu ameanguka dhambin

Akilini mwake utakuta anajisemesha hata sjui kwann mafanya haya yote

sijui kwanini mimi tu

Anatafuta nini chanzo!

Na hamna kitu shetan anapenda kama ukakimbilia matokeo

Kwa sababu matokeo n Jambo la baadae

Na anajua hutakaa ukajua source ya wap imetoka na kwa hvyo utashughulika kwa nguvu nyingi n matokeo baada ya mda unarud pale pale

📖 Matayo:13.54
Na alipofika nchi yake, akawafundisha katika sinagogi lao, hata wakashangaa, wakasema, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii? 

Matayo:13.55
Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda?
 
Matayo:13.56
Na maumbu yake wote hawapo hapa petu? Basi huyu amepata wapi haya yote?
 
Matayo:13.57
Wakachukizwa naye. Yesu akawaambia, Nabii hakosi kupata heshima, isipokuwa katika nchi yake, na nyumbani mwake mwenyewe. 

Matayo:13.58
Wala hakufanya miujiza mingi huko, kwa sababu ya kutokuamini kwao .

Maana yake Nini Yesu alkuwa na haja ya kufanya miujiza kwa lile eneo

Kwanini sababu anasema alipotambua ya kwamba hawaamini hakufanya miujiza kule

Angalia Yesu amepita mahali na mahali amefanya miujiza kbao kakausha miti,, kageuza maji kuwa divai

Sio kwamba hana uwezo kutenda miujiza ila hajatenda kwa kuwa Kuna sababu!

hata ugumu unaopitia Sasa una sababu

Nmekutana na watu wanatembea kwenye mfumo wa maisha ambayo masaa aliyofurahi yanahesabika na masaa amehuzunika ndo asilimia 90 ya maisha yao ya kila sku

Ukikutana nao utashangaa Sana hawana furaha na wanajarbu kutoka huko wakifika sehemu wanajikuta wapo pale pale

Mimi sijui ni ugumu wa aiana gani ulionao

```Ni uchumi, ni kifungo cha tabia, ni uzinzi, ni mahusiano, ni wazazi wako ni ugumu gan uliobana maisha yako kwenye angel```

sijui ni eneo gani limekuwa na ugumu lakini nataka nkuletee hapo badae sababu kadha wa kadha za kwann unapitia ugumu unaopitia

 1.Aina ya watu na Aina ya taarifa unazoruhusu ziwe sehemu ya kufanya kwako maamuzi ya kila siku

➡Nakupa mfano

Nimewahi kutana na mtu aliniambia akiwa darasa la saba aliawahi soma makala moja ikisema kama kijana ukiwa katika hatua za kupevuka njia pekee ya kukusaidia usianguke kuzini n kujichua

Na akasema alijarbu kufikr mihemko ndo imeanza kusumbua mwili wake akaona kapata msaada!

Kwel akaanza kujichua

Till then amekuwa akitembea na huo mfumo

Shida inakuja baada ya kugundua ya kuwa anafanya Jambo litakalo harbu baadae yake yoote

Na amefika level ambayo inabidi Mungu aingilie kati ili achomoke kwenye hilo tatzo

Chunga Sana unayoyasikilza

Chunga Sana unayoyatazama 

Taarfa zinazoingia ndan yako zina nafas kubwa Sana kukuinua au kukuangusha

📖1 Wakorinto:15.33
Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema .

Chunga Sana watu unaozungumza nao

Ni mambo gan mnayazungumzia mara Kwa mara

Wanakumbia wewe n hvyo hvyo huwez kutoka hapo

Mazungumzo yana nguvu ya kubadilisha tabia ya mtu

Yanauweza wa kuiharbu tabia njema ya mtu

Kuna kinds za magumu tunakuwa nazo kwa sababu tumezikarbisha wenyewe

Ugumu kama vifungo vya tabia mbaya kama zinaa, matusi, nk nk

Waulize walioenda jeshin watakuambia

Kwa sababu walkuwa tangu wanaamka mpaka wanalala wanasikia matusi tuuy lugha zao na tabia zao ghafla zkachange

Unajkuta kwa kule kutukana n normal tu kwann

Mazungumzo /taarfa znazotembea ndan mwako mara kwa mara

```Sababu zngne ntakuletea wakat mwingine uwe na wakat mwema``` 
 ```AMEN

No comments: