Sehemu ya 2
....... Tuendelee tulipoishia
➡ Tuliona sababu kadhaa za Kwann Mungu anataka tuenende kwa Roho
➡Sababu inayofuata
2⃣ ili atusidie kuomba yale tunayotakiwa kuyaomba kwa wakati huo
📖Warumi 8:26
kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa
➡ Tafsiri yake ni kwamba kuomba sio tatzo
➡ Unaweza ukaomba na ukaomba vbaya
➡ Au isivyokupasa
➡ Sasa kuendenda kwa Roho inakupa upako wa kufanya Maombi ambayo Mungu akiyasikia anakuwa na priority namba moja kuyajibu
➡ ```Udhaifu unaozumgumziwa ni wa namna mbili
moja si rahisi kwa jinsi ya mwili kuomba kwa muda mrefu kwa sababu mwili ni dhaifu na
pili udhaifu tulionao ni kushindwa kuomba jinsi inavyotupasa kuomba.
```
➡ Ma hapa tunatakiwa kujiuliza swali namna ipi tunatakiwa kuomba kwa usahihi/Au itupasavy0 Ni kivipi
➡ Sasa tunapoongozwa na Roho, maana yake moja anatusidia tuweze kuomba na zaidi anatufundisha namna ya kuomba na kutuongoza yapi tuyaombee kwa wakati huo au kipindi hicho
➡ Mfano wewe unaweza ukawa unaomba upako wa Roho Mtakatifu katika huduma na yeye Roho Mtakatifu, anajua kwamba ameshakutia mafuta na shida uliyonayo ni kutokujua namna ya kushirikiana na upako wake ulio juu yako. Hivyo yeye atakuongoza kuomba kwa habari ya kushirikiana na upako aliouweka juu yako. Kwa kifupi yeye kwa sababu ndiye mwenye maisha yako atakuongoza siku zote kuomba yale unayotakiwa kuyaomba kwa majira hayo iwe kuhusu masomo, ndoa, kanisa, nchi n.k.
3⃣ ili atuongoze katika kufanya maamuzi sahihi juu ya Maisha yako
📖 2Wakorinto 3:17
Basi Bwana ndiye Roho, walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru
➡ Uhuru wa nin Uhuru wa kimaamuzi unakuwa na free mind
➡ *Undirstubled mindset* unakuwa unaamua huku ukiwa unatambua matokeo ya ulichokiamua
➡ Hauamui kwa sababu ya pressure yoyote,,si kwa sababu uingne eyote mbali na muongozo wa Roho kuamua uamuavyo
➡ pia ukisoma warumi 8:1-2 inasema
*sasa, basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu, kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti*
kwako
➡ kufanya maamuzi ni sehemu ya maisha ya mwanadamu
Yapo maamuzi mengi sana ambayo mwanadamu anatakiwa kufanya na hawezi kukwepa kuyafanya
➡ Sasa Mungu kwa kulijua hilo ametupatia Roho Mtakatifu ili atusaidie katika kufanya maamuzi
➡ Roho Mtakatifu anapokuwa Bwana kwako, yaani mtawala, kiongozi ndipo anapokupa uhuru juu ya kufanya maamuzi katika maisha yako
➡ Maana yake ulikuwa hujui nifanye nini? Niamueje ? Sasa yeye anakuletea uhuru ndani wa kufanya jambo ambalo anajua ni la mafaniko kwako
Kumbuka siku zote nia ya Roho ni uzima na amani
➡*```Huenda ziko sababu nyingi ni kwa nini unatakiwa uenende kwa Roho, lakini hizi tatu ndizo Mungu alizonipa tuweze kushirikiana kujifunza. Ni imani yangu kwamba utakapoamua kutaka na kupenda kuongozwa na Roho ndipo utakapoona Mungu akijifunua```*
Ubarikiwe kwa kufwatilia somo 🙏🏿
No comments:
Post a Comment