Popular Posts

Sunday, December 15, 2019

UMEJIANDAAJE SIKU ILE IJAYO/ARE YOU PREPARED?

Part 1⃣
Elikado Mwasenga
  
Somo lenye kichwa umejiandaaje siku ile ijayo/ Are you prepared?

Kujiandaa kwa ajili ya mwisho wa miisho yote tuanze kwa kutazama maneno haya kutoka kwenye maandiko matakatifu,,,


 πŸ“–1 Petro:4.7
Lakini *mwisho wa mambo yote umekaribia* ; basi, *iweni na akili , mkeshe katika sala.

✝ Naomba usome kwa utulivu maneno haya

✝ NLT Bible. 1 Peter 4:7
[7] The end of the world is coming soon. Therefore, be earnest and disciplined in your prayers.

πŸ“– 1 Peter 4:7 But the end of all things is at hand : be ye therefore sober, and watchful unto prayer

Kumbuka Jambo moja maneno haya yaliandikwa miaka zaid ya efu1 na miatano ilyopita

Lakini wale walioyaandika walikuwa serious nayo kuliko watu wa kizaz hiki tulichonacho

Tutatembea Sana na kifungu hiki Roho Mtakatifu atakupa ufunuo na Siri zilizopo kwenye hiki kifungu za kukujenga

 Nianze tu kwa kusema kwamba kila Jambo huwa linakuwa na starting point yake na ending point yake

Mwisho ninaozungumzia hapa n mwisho wa miisho yoye

Yaani n muda ambapo ulimwengu wote na shughuli zake utafikia kikomo!

Nataka uone namna shetani anatumia maonyo hayo hayo ambayo Mungu ameachilia juu ya waamini kuwafanya wasione uhalisia wa kile Mungu anataka waone

Ngoja nkufikirishe kdgo

Unayaamini maandiko kwa kiwango gani??

Soma na Mimi mahala hapa alafu unjibu kwa kiwango gan unaamini maandiko na kile unachokisikia kwa watu

πŸ“– Matayo:6.33
Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

 Nadhan wengi tumewah soma maneno haya

 Nimewahi sikia watu wanasema ukijikuta hautafuti connections unategemea tu imani huna akili lkn maandiko yananiambia hivi utafute kwanza ufalme na haki yake

 Nsiende mbali sana

 Ngoja tuanze kutazama Siri zilizopo hapa kwenye kitabu cha Petro

Jambo la kwanza ninaloliona hapa biblia inakubali kabisa kwamba mwisho upo Mimi sijui Kama wewe unaamini au haumini

Lakin maadamu tu maandiko yamesema hvyo mm nalipokea na kukubaliana nalo bila Shaka hata kidgo

Na anasema very soon n karbu mno

Kama wakati anaandika miaka efu2 ilopita alisema n soon how about today?

Sikia Jambo lingine ninaloliona hapa ni hili iweni na akili(watchful) mkeshe *KATIKA* sala

Maana yake n kwamba n majira ambayo kaama tutaenda tu katika sala au kuomba alafu hatuna akili(taarifa sahihi za NENO LA MUNGU) kuna mahala tutakwama

Maana yake pia n kwamba kadiri tunavyozidi kusogelea miisho ndvyo tunayahitaji maombi na taarifa za neno kuliko kipindi kingine chochote

Shetani kwa kulijua hili angalia alichokifanya kwa wana wa Mungu

 Alipogundua kanisa linatakiwa lishughulike na ufalme wa Mungu kwanza akapachika mahubir ya mafanikio kanisani kias ambacho Wana wengi wa Mungu wanajikuta wanashughulika na mafanikio ya kiuchumi kuliko roho zao

Kuna mtu hajanielewa sipingani na maandiko yasemayo tunatakiwa kuwa matajiri rahasha.........
 Nielewe

Namaaanisha protocol inatakiwa kuzingatiwa

Sipo hapa kuchambua dini au kanisa nakupa neno la biblia

Angalia leo hii semina unazoenda zinakuunganisha na Mungu kuandaa moyo wako kwa ajili ya hukumu?

Au zinakuandaa kukufanya kuwa tajiri lkn hawez kuongea na Mungu Wala hana mahusiano binafsi na Mungu?

kwanini unabii mwingi now days iwe ninaona gari linakuja kwako naona unajenga nyumba

 Cjakataa kuwa hayo Mungu anaweza kufanya

Lakini sitaki kukubaliana nawewe kwamba Mungu atakuletea unabii wa kununua gari na anajua hata ukifa hapo huendi mbinguni

Unasema kwann

 Angalia maandiko yasemavyo

 Kuokoka kwa mwenye dhambi mmoja ni Furaha kubwa mbinguni na jeshi la malaika waliopo kule

Umewah soma mahali maandiko yanasema kununua gar au kujenga kwa mtu mmoja n furaha kubwa mbinguni nionyeshe iyo sehemu

Nataka unielewe vzur

 Ipo hvi mafanikio ya kiuchumi nk nk yanatakiwa kuwa matokeo ya mahusiano yako na Mungu

Mpenzi ufanikiwe Kama roho yako ifanikiwavyo.

 Angalia kuna watu wanajua ahadi za kufanikishwa tu akn hana uhakika kabisa Kama Yesu akishuka hapa Leo atakuwa kwenye kundi lipi

*Are you prepared?*

*Neno linasema utafuteni kwanza!

Kwanza!

```Una uhakika Yesu ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako?```

 ```Unao uhakika na kesho yako ukifa leo wapi utaenda?```

Anasema iweni na akili mkeshe

Na si kukesha tu lakni katika sala

You pray while watching through the revelation of truth

 _Akili_ 
 _Kukesha_
 _Kuomba_

 Soma na Mimi maandiko hayaπŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏ

πŸ“– Matayo:15.8
 Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami . 
Matayo:15.9
 Nao waniabudu bure,

Now days watu wanaenda kanisani sio wakasikie Mungu anasema nini juu ya roho zao wanataka kutabiriwa lini atajenga Lin ataoa  we need to go back to Anguish of God

Anasema amesikia myasemayo kwa midomo, kuimba kwenu amesikia na hana tatzo navyo shida ipo kwenye eneo la moyo kwa sababu mioyo iko mbali naye

Yaani wayasemayo na yale yameujaza moyo n vitu viwili tofauti

Yaani n waamin kwa kuonekana kwao but infact mioyo yao ipo mahali kwngne

Kuna kitu kimekaa kwenye nafas aliyotakiwa kukaa Mungu

Are you prepared?

Haujiulizi n maeneo machache Sana leo hii wamekaza kufundsha watu watafute mahusiano binafsi na Mungu?

Now days kuna mahala haina haja ya wewe kuomba kwa sababu mtumishi ataomba aje akupe unabii imetoka ?

Ukiona umekaa mahali haufundshwi kuwa na mahusiano binafsi ya Mungu mahala hapo hapakufai hapakuandai na mwisho wa miisho

Hembu tufike mahala tuanze kujua kile Mungu anataka tukiishi

Moyo wako umeuelekeza wapi?

Una uhakika Yesu ana nafasi ya kwanza?
Are you sure?

Shetan alipojua unahitaji akili ya maandiko maarifa ya neno ili upate akili za kila Aina za kichwani na moyoni akakufanya uamini haujitaji kusoma neno unahitaji unabii tu na kuombea ili utoke hapo kwenda hatua ingine
My friend tutakupoteza

Anasema iweni na akili!

Iweni makini iweni waangalifu

Kwa tafsir hiyo kuna mahusiano makubwa Sana kati ya mwisho na akili yako

Unasema kivipi angalia maandiko haya!

Matayo:24.38
Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, 
Matayo:24.39
wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

Ukiyasoma vzuri maandiko haya utagundua kwamba watu wa enzi za Nuhu walikuwa wanaendelea na maisha ya kawaida ya kila siku

Kiasi ambacho kwa akili ya kawaida mtu hawezi kugundua Kama kuna jambo linakuja
Akili zimelala

Anaposema iweni na akili anajua kabisa ya kwamba kuna hatari ya kupumbazwa na kawaida ya dunia hii ukaona Kama hakuna kinacho endelea lkn infact muda upo mwishon

Sasa ili uweze kusoma majira na nyakati hizo unahitaji akili ya ziada ambayo utaipata kwa neno la ufunuo wa Mungu juu yako!

Amka amka
Naomba kwa leo tuishie hapa kipindi kijacho nitaanza kukuonesha mahusino ya hivyo vitu vitatu na mwisho wa miisho*
 ```Akili 
Kukesha 
Kuomba```

No comments: