Popular Posts

Wednesday, October 7, 2020

KINGDOM WEALTH CREATION SECRETES

Part2 

Kipind kilicho pita nilianza kwa kukuwekea msingi wa Neno la Mungu juu ya kingdom wealth creation secretes

nkiwa na maana kwamba kuna Siri ambazo kama mshirika wa ufalme unatakiwa kuzifahamu na kuziishi kikamilifu ili kukusanya Mali na utajiri

Leo tutasogea mbele kidogo!
Kwa eneo kubwa tuliona kama ndani yako kuna deficit ya Neno la Mungu unakuwa kwenye wakati mgumu Sana kuweza kutengeneza mawazo ya kimbingu katika kufikia hatua bora na hatima thabiti

Neno la Mungu lislipokuwa msingi wako wa Kwanza sahau kuhusu kingdom wealth

And I said when we are talking about kingdom wealth you should think beyond having alot of money then if you are thinking of money at least try to think of serious money

kabla sijaenda mbali Zaidi kuna Jambo Roho mtakatifu alipitisha ndan yangu nkushirikishe

Matayo:6.29
nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo


Matayo:6.31
Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?

Matayo:6.33
Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

Kuna ujumbe hapa japo nitakudokezea tukizama Sana we will change the focus of subject today

Mstari wa 29 unatupa akili kujua kwamba swala la kuvaa kwaa suleimani yalikuwa la kustrugle kwako kuna external personality ilibeba hilo jukumu unasema kivip

Maandiko yanasema wazi kabisa ya kwamba hakuvikwa hausemi hakuvaaa au hakujivika vzur badala yake anatuambia hakuvikwa akiwa na maana kuna aliyekuwa anahusika na kuvalishwa kwake

Mm cjui kama unanielewa
And it was God himself

Jambo la pili anaposema tutafute kwanza ufalme wake na haki yake na tususimbuke juu ya nn tule,nn tuvae hajakoseaa ndyo sura ya uhalisia wa kile Mungu anataka watoto wake wakiishi
Sasa angalia kitu shetani anafanya

kumbuka lengo la Mungu n ufalme wake uwe the first priority kwenye moyo wako anacho kufanya shetani anaondoa uhalisia huo ndani yako kaa kuwekaa mazingira magumu Hali ngumu kiuchumi na kwa sababu haujatakaa kutembea na Neno la Mungu la kutosha unaona kama Mali isipotafutwa ukatafuta kwanza ufalmea unafail maisha

Lakin kwa kweli with the kingdom kuna kitu kinaitwa uweza utokao juu kimo ndani ya ufalme!!

Matendo ya Mitume:1.8
Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

Nguvu ya kushuhudia n matokeo ya Roho mtakatifu kukaa juu yako

Mungu hatukupa kushuhudia bila kukupa means na facilities za kukuwezesha kushuhudia!
N vile tuy tunashinda kuelewa kwamba hiyo power inaweza kuwa expressed into various attributes

Unaweza kuwa kama miracle working power

Unaweza kuwa kama wisdom teaching power

Inaweza kuwa kama wisdom for problem solving power

It is the same power but because it is limitless power it can be expressed in various attributes and the goal is to manifest Jesus to reveal the living Jesus we are a proof and evedence that Jesus is God!

The same thing comes at wealth creation
That power also can be expressed as wealth creating power!

Kumbukumbu La Torati:8.18
Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.

bila Shaka kuna point umedaka hapo

So what am trying to do n kukupa ufahamu utakao kusaidia wewe kuweza my unlock that power because it is given to you as potential power for it to bring out results it needs to be unlocked first!

That is why am teaching you these secretes they are kingdom secretes!

Tuendelee na Siri ya pili
2. Kingdom wealth is tied to the value of time

Mafanikio ya kifalme yamefungwa kwenye muda kwa lugha nyepesi muda n Jambo la muhimu la kuzngatia unayotaka kukusanya utajiri ndan ya ufalme

Neno la kiswahili jalijakaa poa utajiri n kakitu kadogo Sana ukilinganisha na kingdom a wealth makosa Neno zur kukutumia hapo ila elewa hivyo

Waefeso:5.15
Basi angalienisana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima

Waefeso:5.16
mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu

Jambo utakalo lionaa kwenye andiko hili n kwamba Moja ya mambo yanaweza kukusaidia kujua kama mtu ana hekima ni mwenendo wake hasa kwenye namna anavyotumia muda!

Ngoja nkupe andiko hili kwa namna pana kidogo

Ephesians 5:15‭-‬16 AMP

Therefore see that you walk carefully [living life with honor, purpose, and courage; shunning those who tolerate and enable evil], not as the unwise, but as wise [sensible, intelligent, discerning people]

making the very most of your time [on earth, recognizing and taking advantage of each opportunity and using it with wisdom and diligence] because the days are [filled with] evil.

Redeem you time

Neno komboa au redeem lililotumika hapo kwenye origin writings n Neno exagorazō usiwaze kama huwezi kulitamka😁😁
Maana yake hilo Neno n
Rescue from loss au kwa tafsri ingine ni

improve the opportunity

Paulo alichokuwa anajarbu kutumbia hapa n kwamba we need to rescue time from loss!
We need to improve the opportunity of time to bring out treasures out of it!

Kwa picha hii napata akili kwamba ndani ya muda kuna agenda maalumu na kubwa Sana imefungwa humo

Now the question is how do you rescue time from loss how do to use time as an opportunity and improve that very opportunity to create kingdom wealth??

1 Wakorinto:14.40
Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu

1 Corinthians 14:40 NLT

But be sure that everything is done properly and in order

In order to redeem time you need a well organized lifestyle
Maisha yaliyipangiliwa yanajisoma

Maisha yawe yanaeleweka unafanya mambo yako kwa muda na kwa wakati!

Time is also important if you want to create kingdom wealth
how to organise your life and your things with regard to time!

Unahitaji mambo makuu kadhaa ambayo yamethibitihswa kimaandiko
Jambo la Kwanza haukuzaliwa ufanye kila kitu hapa duniani you have your own special task

You are a unique specie of your own

Kwa hyo lazima ujue umeitwa kwenye category gan ili ukusaidie wewe kuweka mambo yako kwenye mkakati maalumu!!

baada ya hapo hatua inayofuata n wewe kufanya yafuatayo

1. Invest in yourself work on being muda wako mwingi uitumie kujinoa utu wako wa ndani!

Improve your personality
Nourish your mind nourish your character before you start looking for money before you start looking for investment

Because it is from what is with in you that you are able to birth out!

My question to you is what do you do with your time
What is that which takes the most of your time in the daily basis ??

Unasoma vitabu Kias gan Unasoma Neno Kiasi gan unaomba masaa mangapi
Wengine wanatumia Neno jitafute

Find the best aversion of you
Make sure everyday you are existing as the lastest model of you
USE YOUR TIME WISELY

Unaweza kuwa na mipango mizur maono thabiti lakin kama swala la kutumia muda utalipuuzia hufuki popote nakwambia

Hakikisha hata kama unataka kuanza biashara unataka kufuga hakikisha una taarifa nyingi zaida ya mtu yoyote kuhusu hilo swala and you will see why the Bible demands us to buy the opportunity (time) to redeem(to improve to rescue from loss)

2. Segmentation
Maana yangu n nn
Hapa ninachotaka ukione n kwamba uko na vitu viwili viatati vya kufanya

Let's say wewe n mwanafunzi
Una kusoma masomo ya darasan unahitaj kusoma Neno unahitaji kujinoa juu ya uchumi nk nk

Sasa huwezi kufanya vyote kwa wakati mmoja na kwa ubora sawa

Segmentation is all about categorizing these things into ranks

Unagawanya vipenegele maisha yaliyo pangiliwa yakapangika!

Kinachofuata na hatua ingine

3. Concentration
Hapa unatakiwa kutumia muda wako mwingi kwenye jambo ambalo unataka kuliishi maisha yako mengi
You bring your full concentration to it
You spend much of your time on it!!

That is what we call wisdom for Dominion

Mungu akubariki

Kingdom Wealth creation secretes

Part 1
Ni Maombi yangu kwa Mungu akufungue akili upate kuelewa ujumbe wake maalumu kwako ameN

Jambo la Kwanza kabisa unatakiwa kulijua is that wealth is created and also can be created

```Jambo la pili linatakiwa kuwa ndan yako n kwamba kingdom wealth is beyond money```

Ntakupa Siri chache za ufalme za kukusaidia kucreate wealth as a kingdom envoy
Shalom

Mungu alipokuwa anafanya uumbaji alikuwa anaumba akiwa kwenye nafasi ya uungu inayo itwa Mungu muumbaji(muumba wa mbingu na nchi)
Utaona kwenye kitabu Cha mwanzo kabisa kitabu Cha utambukisho Biblia inaanza kumtafsir Mungu kama Mungu muumbaji

Mwanzo:1.1
Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi

Kwa hiyo tunaanza kumuona Mungu kwenye sura ya mwanzo kabisa Kama Yeye anataka tumjue kama n Mungu anaye umba he is God the creator

kwenye mchakato wa kuumba he spoke words into existence

Waebrania:11.3
Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri

Maana yake n kwamba kitabu cha mwanzo the raw material God used to create was words
Ninachotaka uanze kukiona hapa n juu ya maneno yaliyoumba kabla hayajatika Kuna mahala yalikuwa yana exist

before halijawa Neno la kuumbia ulimwengu lilikuwa Neno la moyoni mwa Mungu Kuna mtu ananielewa hapa?
So my interest is the word in the womb of the spirit of God before he spoke it into existence

This is very powerful mystery
hilo Neno kabla Mungu hajalitamka lilikuwa moyoni mwake!!

Ndyo Mungu huwa na hisia piah

Anaweza kufurahi, anaweza kuhuzunika, anaweza kukasirika kwa lugha hiyo anawaza piah anayo mawazo!

Yeremia:29.11
Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.

Kama huwa anawaza ana mawazo ana mipango maalumu uwe na uhakika wakati wa uumbaji kabla hajasema iwe hiki owe kile vikatokea vilikuwa processed kama mawazo kwanza!
So creation haikuanzia kwenye kutamka ilianzia rohoni kwenye dimension mbali na uhalisia wa uumbaji ulipotokea!

This is all about creation!

So if we want to start creating wealth the first area we need to deal with is in the heart for it is where creation originates

Am talking about kingdom wealth you should be thinking beyond having alot of money in your bank account

tunapoanzaa kuuchakata moyo(nafsi/your mind) tutakuwa naa vipenegele vya kuviangalia

Sasa your mind will always be processing the informations available with in you

Una taarifa za aina gani na kwa kiwango kipi ndani yako vinaamua moyo wako ufanye mchakato(processing) kiasi gani juu ya kingdom wealth!

Kwa hiyo sasa kingdom wealth creation begins with the processing of the information originated from the kingdom with in your heart!

All the required informations are in the word of GOD

That's means kama ndan yako hujaanza kuweka Neno n vgumu kuanza kujua unaanzia wapi kukusanya utajiri wa 
kifalme!

Leo nataka tushughulike na taarifa na moyo/mind ya 
kwako

Nmekuambia kwamba kabla Mungu hajaanza kuumba lilikuwa na wazo!
hili linanipa ujasiri kusema kwamba kile ambacho hauna kina uwezekano wa kuwepo kama tu kinaweza kupata nafasi ndan ya moyo wa kwako

Remember also we were created in the image and likeness of God

Ndani yako kuna hiyo creation ability

Mungu amekuwekea kwa makusudi maalumu
tunachotarajia n moyo wenye uwezo kutafsir mambo kwa kiwango Cha kuweza kucreate wealth!

kwa hiyo Sasa kama kuna maeneo unatakiwa kuwa Makin nayo katika hatua za mwanzo n kuweka kudeposit Neno la Mungu la kutosha ndani yako kwa sababu kwa hilo uumbaji ulifanyika na kwa sababu hiyo likikaa ndani mwako lina Activate that part of God responsible for creation ndan mwako

That's to say in this Kingdom you don't the word of God you can't create wealth,you can never produce anything that 
was never found inside of you

Proverbs4:23
Keep thy heart with all diligence; for out of it are the issues of life.

Proverbs 4:23 KJV
Ukisoma maandiko haya kwa makin utaona maandiko yanaguide kulinda moyo kuliko vyote tunavyovinda na sababy kubwa n kwa sababu kwa huo comes out issue that concerns your life!

What so ever you will demand in this life is in your heart
but there is technology in this Kingdom to bring out those issues in your heart into existence

Una information kiasi gani ndani yako za Neno la Mungu kuhusu wealth creation?

angalia kama MUNGU alikuwa na wazo kabla ya kuumba for us to create wealth in this kingdom we need the right thoughts!
and those thoughts are coming from a the word of God

kwa hiyo unatakiwa kuanza kuilsha nafsi yako neno la Mungu ili likupe uhai kwenye category unayotaka kufanikiwa kwalo(wealth creation)

ndani yako ukiweka Neno la kutoshaa likawa processed aaKwa umakini you will bring out wealth from inside of you
tunapotaka kuproduce daktari what we do is not to give him medicines or Patients no we first induace informations in him that will active his mind to be able to detect and cure diseases!

For a person to be able to create wealth you will need some informations in you to activate that part of you with an ability to create wealth to be active and make the best of out of you

There is a reason for why God gave you a mind!
Kingdom wealth creation
Waebrania:4.12
Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

Your mind needs the word of God for it to be sharp and bring out of yiu the issues of life

Kingdom wealth creation

Ngoja nkwambie kitu
Kuna elikado ambaye afamily yake inamfahamu Kuna elikado rafk zake wa karibu wanamfahamu, kuna elikado watu wanamuona mara kwa mara wanafahamu na kuna wewe unayemfahamu wewe peke yako na Mungu!

There are so many you
but am interested in the you whom you knows alone and God

Huyo mara zote ana ndoto kubwa, ana maono makubwa, huonag inawezekana, huona ukuu akiweka na Mungu wether anajua au hajui ila huwa anaona
Huyo huwa akipanga mambo anaona Raman nzima mpaka mafanikio yake au hatima yake
Huyo haijawahi kuona kufeli
He is a very strong personality

The problem to many of you is the inability to bring out that personality into existence

Your mind is bigger than you know it you just lack the activator for its expression to bring out the best out of you(issues of life)
The word of God

Saturday, September 5, 2020

FRUITS OF PRIVATE PRAYER

Ni maombi yangu mbele za Mungu akupe ufahamu na masikio ya kusikia ujumbe wa somo hili na ukujenge ukupe hatua mpya

Jambo la Kwanza nnalotaka ujue n kwamba Maombi mchakato wa kiroho ambao una matokeo maalumu ukifanywa kwa kuzingatia kanuni za kiroho zilizowekwa

Na Moja ya Mambo utakayokuja kugundua ni kwamba kadili unavyozidi katika eneo lako la kuomba eneo ulilopo linaanza kuunganisha na ufalme wenye mamlaka ya kiungu (wambingu)
hilo eneo linakuwa chini ya utawala wa Mungu unayemuomba na kwa njia ya wewe anaaanza kulimiliki Hilo eneo
remember we are extension of the kingdom of God

We are kingdom envoys

Lakin eneo ambalo nataka tuliangalie ni lile la maombi binafsi

Kwanini nasema hivyo
Kwan hujawahi ona Ukiwa na watu fulani unakuwa na fire ya kuomba au ukienda maeneo fulani unakuwa na nguvu kubwa ya kuomba lakin Ukiwa peke yako unakosa kabisa nguvu ya kuomba!?

This tells me that private prayer inahitaji mfumo binafsi utakao kusaidia kuomba tofauti na mfumo wa kundi kuomba

Na ujue kabisa kwamba eneo unalotumia kuomba Lina uhusiano mkubwa Sana na kiwango chako Cha kimaombi
Ndiyo maaba wengine wakiwa kanisani kwenye vikundi vya maombi wanaomba vizuri Sana lakin wakiwa peke yao nyumbani nguvu ya kuomba haipo tena

Unafikiri tatizo liko wapi?

Listen nguvu ya kuomba huwezi kuiona unapoomba tuy unapoakuwa kwenye kundi nguvu ya maombi utaanza kuiona unapokuwa peke yako nyumbani

The time you are able to connect heaven when you are alone

May be you want to say you are busy

rafik angu,,, Daniel was a busy man alikuwa anafanya Kaz serikalini but he prayed three times a day

Kwanini maombi binafsi kwa wakristo wengi imekuwa Ni tatzo Sana now days???

Private prayer
Kwa watu wengi now days they don't have time to pray alonE!

Unasema kivipi
Siku Moja jaribu kumpigia rafk yako simu Anza kumueleza Mambo ulitaka kumuomba Mungu utakuja kuona lisaa linaisha pengine hujamaliza kumueleza lakin Anza kuomba maombi hayo hayo kwa Mungu Utaona hata nusu saa Kaz kumaliza kuomba

Private prayer is very important lakin ni Moja ya Mambo ambayo shetani anapigana Sana kuhakikisha hupati nafasi ya kuyaishi
Fuatilia maandiko kwa Makini utagundua kwamba ufunuo alikuwa anawapa Mungu kuhusu maisha yao binafsi na kazi aliyompa mtu mmoja mmoja Kama life time assignment walikuwa wanazipta wakiwa wao peke yao na Mungu kuomba

Do you have private time where you are always alone with God??

Na kitu kibaya Zaidi duniani ni mifumo iliyopo makanisa mengi now days am not doing this to criticize but to build swala la kuwa mtegemezi kwa nabii wako, mchungaj wako, mtume wako Kias kwamba hauhitaj maombi binafsi huo ni ugonjwa

Me I call it spiritual paralysis

watu hatuombi!!!!
Usizunguzmie maombi ya kanisani kwako najua utasema aisee yalikuwa fire balaa
Swali langu kwako ni je iyo fire unaiona Ukiwa peke ako kwenye madhabahu yako ya maombi nyumbani???

Na wengine kwa kudanganywa na giza la ulimwengu huu wakiwa kanisani wanatembea kwenye mihemko wanalilia uongo ila kwa kweli wanajua Hali yao ya kiroho haiko sawa
Am talking about Fruits you should expect from your private prayers

Revelations comes from your prayer alter when you are alone with God

Matendo ya Mitume:2.1
Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja

Matendo ya Mitume:2.3
Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao
Ukiangalia maandiko hayo utagundua kwamba pamoja na kwamba Hawa jamaa walikuwa mahali pamoja lakin kila mmoja alipokea ujazo wa Roho Mtakatifu kivyake anasema zile ndimibza Moto zilimkalia kila mmoja wao yaan kila mmoja alikwa na ulimi wa Moto kivyake juu Yake!!!
Am talking your personal life bro
Matendo ya Mitume:10.3
Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio!

He was alone when he met God!!!

Kama hauna maombi binafsi Kuna tatzo mahali
kama haupati muda peke yako kuomba kuna shida mahali
Kasome Biblia yako Utaona kabisa kwamba hakuna mtu ambaye Mungu alintumia kwa viwango vikubwa namaanisha viwango vikubwa (transgenerational pillars)  ambaye hakuwa mtu wa maombi binafsi( men of secret prayers)

Hayupo Kama yupo Basi Mimi nimesoma Biblia iliyo forged
You want to see an anointed personality in your life??
Have a regular daily intense time of prayer with God!

```Unalala masaa yote 
Unakula will nzima 
Forget about the anointing of God```

God does not give his anointing to lazy Christians never

Una muda binafsi wa kuomba???

Lazima uwe na muda binafsi wa kuomba namaanisha Lazima Kama unataka kutumiwa na Mungu
Private prayers will tell you how weak you or how strong your are!!!

Ukitaka kujua ulivyo angalia eneo lako la maombi binafsi
Have I come to realize Eliya hakuwahi kuwa na Zaid  masaa24 but his Prayers we're amazing one

Muda wako wa maombi Ni wa maana Sana kuliko unavyofikiri

You don't pray forget to be used by God

Maombi binafsi(private Prayer) yanakupa kujua upo dhaifu kiasi gani au imara kiasi gani katika Mungu
Let me show you something
Mtu yeyote anaweza kusoma Neno mtu yeyote anaweza kufundisha na kuhubiri lakin si kila mtu anaweza kuomba!!!

Nisikilze kwa makin ni eneo la maombi peke yake Tena maombi binafsi achana na ya kundi ambapo Unaweza kuona uhai wa maisha yako kiroho!!!
Kuomba n kujitoa

Kuhubiri,kufundsha yanaweza kuwa matokeo ya vitu unavyovifahamu
Maombi hayahitaj misiamiati mitamu mitamu ili yawe maombi serious yanahitaji Moyo ulio pondeka na kunyenyekea

It is only in the place of prayer where God will break you down and you bow before him the Ancient Zion King!!!

Isaya:66.2
Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema Bwana; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu

Angalia anachosema Mungu anasema kila kitu unachokiona amekiumba yeye mwenyw ndye aliye kiumba!
Lakin jicho lake linaangalia watu kadhaa kwa lugha nyepes n Kama anataka kusema watu ambao huwa nawatazama kwa ukaribu n mtu mwenye roho iliyopondeka ba ndan yake anajikuta amenyenyekea neno la Bwana linaposikika!!!

Sasa sikiliza si watu wote huwa wakilisikia neno la Mungu linakuwa na uzito ndan ya mioyo yao

Oooh my God sijui Kama unaona kitu nataka uone hapa
Maana yangu n kwamba mtu mwenye maombi mengi huwa kwenye mazingira ambayo neno la Bwana linaposikika the word hits his inner being directly

Iko hivi maombi yanachokifanya sio kumketa Mungu karibu yako hapana badala take yanakusogeza wewe karibu na Mungu Sasa ukaribu huu usifikrie ule was kusema npo mbali kilometers kadhaa nooooo 


Ukarbu huu n ule wa wewe kuwa na uwezo wa kuinteract with and share the life of God unakuwa unauishi uhalisia wa kiungu you become concious of God's presence in your every day Life
Maombi yanakupeleka kwenye ulimwengu mwungine mbali na uhalisia wa dunia hiii 
When you begin to pray you begin to travel in the spiritual realm!!!! 

You travel to the world with boundless entity
The world of the spirits

Mtu mwenye maombi I mean seriously prayer man anauwezo wa kuiona ajali ya mwezi ujao mipango ya giza ya wiki kesho na kwa njia ya maombi akageuza ule ubaya

Anaposema faith is a substance of things hoped for ana maana kwamba in faith dimensional world(spiritual world) you touch the substance of what you are hoping Kama kuna Jambo unalitumainia unalitarajia it is through prayers and faith you touch that thing a substance of things hoped for!!!!!

Yaan kwa Imani unakuwa unakishika kabisa hicho kitu rohoni prayer men can do that and beyond!!!!

Mtu mwenye maombi mengi yanayotokea huku duniani hayawezi kumshawishi kuachana na kile anachokishika rohoni(substance you hope for) kwa sababu n halisi kuliko material world !!!!

TUNAENDA SAWA SAWA!!??
Nisikilze private prayer is mandatory if you want to go far with God

Ngoja nkuonyeshe Jambo la ajabu kidogo

Waebrania:5.7
Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu

This was the life of Jesus
Maandiko yanasema alimtolea MUNGU maombidua na kulia kwingi

If this was God in the flesh and his prayers was like this how about the young people like you and me???

No wonder wanafunzi wake pamoja na kuona akifanya miracles zote zile maajabu yote Yale walichokiomba kwake n Bwana tufundishe kuomba!!!

Maana Yake nini
Wanafunzi wake walikuwa wakiyaona maisha ya Yesu the man was always speaking with spirits through prayers wakajua the screte about his powers and miracles is the world he was interacting with frequently it the heavenly realm

It is only men prayers who are able to travel to this dimensional kind of life !!!!
The other man was John the beloved
Yohana wa kitabu Cha ufunuo!!!

Nlikuwa nkifuatilia historia yake utakuja kugundua kwamba yule jamaa alikuwa n maombi kiasi ambacho hata kifo kilikuwa kinagoma kumchukua he became like one among the cherubim!!!
Walitaka kumuua yule jamaa
Walimuweka kwenye lami iliyokuwa imechemka vibaya lakin jamaa hakufa Wala kupata dhara lolote

Wakamfunga na farasi huku na huku kumvuta akatika vipande vipande but death refused to take him!!!
Ooooh glory glory!!!!

Wakaamua kumpeleka kisiwa kiitwacho patmo( the island of Patmos) ili afe na njaa matokeo Yake tunakuja kuona Yohana anaema nalikuwa katika roho oooooh my God these are men of prayers serious prayer meN!!!!!
Nisikilze praying is a sucrife broh

Huonagi ukitaka kuomba dakika ishirin zinakuwa Kama mwaka

Njoo kuchek movie Sasa masaa10 yanakuwa Kama dakika 5

We need God everyday some more 

THE FRUITS OF PRIVATE PRAYER

Tunapokuwa tunamuomba Mungu,,, Mungu anakuwe wetu yeye na uungu wake wote!!!

Andrew Murray Aliwahi sema 
Mungu anaweza kila kitu
Kwa lugha nyepesi maombi yanaweza kila kitu

swala la kuomba limekuwa tatizo  Sana kwa kizazi hiki
Mungu atusaidie Sana
Leo hii ukikutana na mtu alienda dry fasting hata ya siku tatu Ni wachache Sana  because we don't know what prayer can do to your spirit!!!!

Yakobo:5.16
Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii

Sio tuy swala la kuomba ila kuomba kwa bidii ndiko kunakofaa!!!!

Luke 18:1 KJV
And he spake a parable unto them to this end, that men ought always to pray, and not to faint

we are Beings of prayers

Binafsi nlifanya maamuzi I will pray like never before I will fast like never I want my generation to one day say we thank God for you

I decided to be a creature of fasting and prayers

I have seen God in my knees great things in the secrete place with the Lord

ThE DEVIL IS IN TROUBLE

 
Kingdom teacher,preacher

Elikado Mwasenga
0716333958

Friday, May 15, 2020

MUNGU ANATAFUTA MTU WA KUMFUNUA DUNIAN

Bwana Yesu asifiwe Sana mtu wa Mungu  
Karibu tena tujifunze neno la Mungu

Ngoja nkutazamishe jambo hapa kabla cjaanza kuelekeza somo letu
Kwa wale ambao wanaifahamu Unaweza ukanielewa kwa haraka lakini 

 Crude oil 
Is complex mixture of hydrocarbons

Sasa ikiwa katika complex form huwa haina msaada lakini ili tuweze kupata faida ndani mwake lazima tuipitishe kwenye refining system ili tuweze kupata attributes tofauti tofaut Kama petrol , disel nk nk

Vivyo hvyo Mungu amejiweka katika mfumo ambao n very complex tunaitambua Kama (Holy spirit)

```Sasa Roho Mtakatifu yupo kwenye mfumo ambao n very complex lakin ili watu wa kawaida ya duniani wamuone katika uhalisia wake lazima kuwe na mchakato Fulani ndani yako ambao utamsaidia kujifunua kwao!!!```

Moja ya vitu ambavyo utakuja kugundua Ni kwamba Mungu huwa hafanyi Jambo lolote duniani bila ya kumpata mtu Kati wa kumuunganisha na mifumo ya huku ulimwenguni!!!

Nilifikir kwa kina
Alipokuwa amechukizwa na maovu ya watu wa kizaz Cha Nuhu hakutoa adhabu Moja kwa moja alimtumia Nuhu!!!
Alipokuwa anahukumu maovu ya kizazi Cha Sodoma na gomora alimtumia Luthu na Ibrahim!!!

Kwa mawazo yangu ya haraka haraka ilinipa ugumu kukubaliana na hali hiii yeye Kama Mungu muweza wa yote kwann asiwapige moja kwa moja kwa uweza wake

Si hivyo tuy wakati anataka kuwatoa wanna wa Israel kule misri hakuenda yeye Kama Yeye lakini sisi tunajua kabisa ya kwamba Ni Mungu ndye aliwaokoa!!!

Narudia Mungu anatafuta mtu wa kuelezea uhalisia wake katika Angle tofauti hapa duniani!!!

Child of God nielewe vzuri Mungu anataman sana tuone uhalisia wa uweza wake katika maisha yetu ya Kila siku!!!
Warumi:8.19

Kwa maana  viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu

```Uwe na uhakika kufunuliwa kwa wanna wa Mungu sio swala dogo kwa sababu kufunuliwa anakozungumzia Ni kule kuExpress a certain dimension of God```

Maana yangu n kwamba Kuna kitu Kinatakiwa kitokee kwenye maisha yako ya Kila siku ambacho sis tukikiona tumuona Mungu ndani ya maisha yako

Naomba tusome kitabu Cha matendo 1;8

Watu wengi huwa wanalielewa hili andiko katika Kona ya nguvu za kufanya miujiza na kutoa mapepo tuuy!!!

Lakin kwa kweli Nguvu hi ya kiungu ipo katika Kona nyingi Sana
Ndo maana nimekwambia Holy Spirit is in a very complex form!!!

Kwa mfano ngoja nkutazamishe maandiko machache
Luka:16.20
Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, 
Luka:16.21
naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. 
Luka:16.22
Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.

Ukisoma kwa makini habari hizi utagundua Kwamba Lazaro alikuwa hana utajr wa Mali ila alikuwa na utajiri wa upako au kwa lugha nyepesi alikuwa mtu wa kiroho usivyoweza kudhani na ndiyo maana Utaona kwamba the moment amekufa yupo kifuani pa Ibrahim ikiwa na maana kwamba maisha yake yote huyu jamaa aliiish kwa iman ya kufika mbinguni!!!

Na Utaona kabisa role model wake alikuwa Ibrahim yaan alikuwa anaishi maisha ya imani Kia's ambacho alifikia level za kuwa na iman inayofanana na ya Ibrahim
Ooh nataman uone hili jambo
Angalia Jambo lingine

Luka:4.14
Yesu akarudi kwa nguvu za Roho akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando

Hapa ni Yesu akiwa ametoka kwenye mfungo wa siku arobaini mfululizo bila kula chochote!!!

Kwa hali ya kawaida alikuwa kaishiwa Nguvu mwilini lakin kwa Nguvu ya Roho Mtakatifu alikuja na uzima!!!

Kwa hyo hiii Nguvu ipo kwenye dimensions tofauti tofauti!

Kumbukumbu La Torati:8.18
Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.

Ni Nguvu ile Ile ya matendo 1:8 hapa ikiwa inaelezea dimensions ya kupata itajiri!!!
Kwa sababu bado Ni kwa ajili ya ufalme!!!

Nataman upate picha halisi hapa
Sasa Kuna category tofauti tofaut za kuelezea uhalisia wa Mungu(kumfunua Mungu) duniani


Your life can be a blessing and a dimension God's ability on Earth!!!

Jambo la kwanza unalo hitaji Ni Power of the Holy spirit
ngoja nkuoneshe andiko kidogo

Matendo ya Mitume:10.38
habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.

Hapa nataka uone Mambo mawili ya muhimu
Jambo la Kwanza kumtia mafuta(to anoint) by the holy spirit

Jambo la pili Ni kumtia mafuta(to anoint) kwa Nguvu by power (dunamiss    power)

Ukitazama kwa makini Utaona Kuna Mambo mawili yanahitaji kutokea ili mtu aanze Kimtambulisha Mungu mahali kwa viwango ambavyo anakuwa Ni halisi kwa Kila anayekutazama wewe

You need be anointed by the person of the Holy spirit (his personality to be yours)

To anoint is to be given an authorization over something

Tunaposema Mungu amekuAoint it is something like umepewa nature ya namna ya kiungu ambayo kwa Namna ya kawaida usingeweza kuwa nayo
Ngoja nkuelezee kidgo hapa

Isaya:61.1
Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu;  kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao

Ukisoma andiko hili Utaona kabisa huyu jamaa alikuwa n mtumishi wa Jehovah lakini kabla Roho wa Bwana( Roho Mtakatifu) hajakaa juu Yake hajawa sehemu ya utumishi wake Kuna Mambo alikuwa hana uwezo wa kuyafanya lakini alikuwa mtumishi wa Mungu!!!

Lakn baada ya mchakato wa kuwa anointed kinachotokea anaanza kuOperate supernatural things in a natural rhealm

Anasema amenipaka mafuta(he has anointed me) to do something!!!

Kwa lugha hiii utagundua Kwamba kuwa anointed n kupewa uwezo ambao umebeba uungu na Umungu ndani mwake

Turudi kwenye point yetu ya Kwanza anaposema kupakwa mafuta kwa Roho Mtakatifu na kwa Nguvu

1. Roho Mtakatifu nilianza kukueleza he is a very complex personality
Kwa hiyo anapokuwa introduced ndani yako yaanzi tu kuyaendesha maisha yako
He is a very gentle personality as well
Anahitaji ruhusa yako kuyaendesha na kuyaongoza maisha yako

Sasa anaweza akawa ndan yako na bado ukashindwa kumfunua Mungu mahali ulipo kwa sababu Kuna mchakato haujachukua nafasi ndani mwako

Ngoja nkueleze Jambo hapa
Roho Mtakatifu anapokuja ndani mwako kiu Yake kubwa Ni kukufanya wewe kuwa wake kwa maana ya Kila kitu kuhusu wewe kuwa under his authority lakin kwa ruhusa yako

Anataka akupitishe kwenye mambo kadha kadhaa ili Sasa aanze kukutumia Kimtambulisha Mungu kwa watu waliopo kwenye hilo eneo!!!

Eneo la Kwanza analoanza kushughulikia n utu wako wa asili au tabia zako kwa lugha nyepesi

Kwa sababu tuliona mtu wa asili hawezi kupokea Mambo ya Roho wa Mungu
Ndyo maana kuamka usiku kuomba sio swala la kimwili you need to be empowered by him

Swala la kutokasirika ovyo ovyo swala la kutojadili watu badala ya Yesu madhabahuni n swala la kiroho Sasa Kama Ndani yako haja shughulikia ipasavyo huwezi Kimtambulisha Mungu !!!!

Ngoja nkupe mfano
Yohana mbatizaji maandiko ynatuambia alijazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama Yake

Ila kilichonipa shida kuelewa n kwann hakuanza moja kwa moja kumfunua Mungu kwenye eneo alilopewa Kimtambulisha Mungu!!!?

Nkaja kuona huyu jamaa alikaa jangwani(nyikani) kwa muda mrefu Sana na maandiko yanatuambia alikuwa akila asali na ngize n mazingra Magumu Sana haya!!!

Na Nina uhakika Roho Mtakatifu alimpeleka kwenye mifungo na kuomba kwingi mno katika hicho kipindi
Kwann kwa sababu moja ya Mambo Roho Mtakatifu atafanya n kuhakikisha anaua utu wako wa asili(your flesh) kias ambacho Roho yako inakuwa dominant kwenye Kila kitu kuhusu wewe
Na Utaona Yohana alikuja Yordan Biblia inasema nji nzima na zote zilizokuwa kando kando walimjia kumsiliza
This is a result of being anointed!!!

Kuna watu wanashindwa kutofautisha Kati ya kuwa imparted na kuwa anointed!!!
Sikilza huyu jamaa alikuwa kashaa zalisha upako Kia's Cha kuhudumia mataifa your hayo!!!

Hapa uwe na uhakika alikuwa hajitazami yeye alikuwa n krsto ndani mwake(Roho ndani mwake)
God is all he lived for!!!!

Nadhani umenielewa kwamba kuwa na Roho Mtakatifu Ni Jambo moja kutembea katika utu wake au kutembea naye n Jambo lingine you need fasting and prayers non ceasing ones
Mungu anataman kuona unamtafuta Kias ambacho he will make himself known to you!!!

Jambo la pili to anoint by power Ni matokeo ya wewe kutembea na Roho Mtakatifu mpaka anakuwa yeye ndiye Nguvu yako ndye maarifa yako ndye Kila kitu chako he becomes the all that you have!!!!

Matendo 1;8

Monday, May 11, 2020

JIZOEZE KUTAFSIRI MAMBO KIROHO ILI UTEMBEE KWENYE UKUU WA KIUNGU


Kwanini ninasema hivi
Kwa sababu nimekuja kugundua kwamba Kuna Mambo mengi Sana amabyo Mungu hutaman yatufukie kwa wakati lakini huwa inakuwa vigumu sisi kuchukulia uzito kwa sababu tunatembea Sana na mitazamo ya kibanadamu kuliko tunavyotafsir kiroho

Kuna Mambo ukiyatazama kwa namna ya kawaida huwezi kuona mpango madhubuti wa Mungu ndani yake

Umewahi kujiuliza kwann Paulo alikaza Sana kuombea kanisa la Efeso juu wao kuwa na namna ya kiungu ya kutazama mambo!!!

Waefeso:1.18
macho ya mioyo yenu yatiwe nuru mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;

Ukitazama kwa makini Utaona kabisa msisitzo wa Paulo upo kwenye uwezo wa mioyo yao kuona

Kumbuka kuona kwamba moyo Ni pamoja na Namna mtu anavyo uafasr Mambo anayokutana nayo Kila siku
Anasema macho yatiwe nuru(yapewe uwezo/power) to see in Godly way the things of our everyday lives

Kwann macho yatiwe nuru(ya kiungu)

Tazama maneno haya
1 Wakorinto:2.14

Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni

Maana yake nn
Tafsr Yake n kwamba kuna vitu vingi Sana Mungu huwa anavipitisha kwenye maisha Yetu ya Kila siku na tunayaona kwa jicho la asili(kibinadamu) na kwa sababu hiyo tunakosa uwezo wa kuona kitu au faida za kiroho(kiungu) zilizomo ndani mwake

Nataman nikitazamishe Mambo kadhaa kwenye maandiko uyaona kwa undani

2 Wakorinto:4.4
ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.

Ukitazama tofauti ya mtu mwamini na mtu asiyemwamini n utendaj Kaz wao wa utu wa ndanj
Kuna mmoja ana Fikra zinazoona Kiroho Kuna mwingine ana upofu hawez kuona Kiroho

Maana yake n kwamba katika uhalisia wa kiungu haoni chochote anaona uhalisia wa Jambo hilo kimwili ambalo kwa kweli Lina uhalisia mkubwa Zaid Kiroho kuliko mwilin anakoona yeye

Ngoja nkupe mfano
Bila Shaka umewah kusoma habr za kuzaliwa kwake mwokozi(Yesu) katika kitabu Cha Mathayo

Ngoja tutazame kwa pamoja
Utaona kabisa Yusufu na marina walikuwa kwenye hatua ya uchumba
Lakin Cha ajabu Mariam alikuwa tyr ana mimba ambayo kimsingi sisi tunajua kabisa n matokeo ya Roho mtakatifu kuja kutimiza kusudi maalumu

Na Jambo lilinishangaza Ni kuona Namna Yusufu alivyo fanya maamuzi juu ya mimba aliyoiona kwa mchumba wake na kwa kweli haikuwa ya kwake na hakujua n ya nan
Maandiko yanasema akaazimu moyoni mwake  kumwacha kwa Siri

Kwann kwa sababu alikuwa mtu mwenye haki(mtu wa kiroho) Kia's ambacho pamoja na kwamba mchumba wake ameamua kumasaliti lakini hakutaka kufanya liwe Jambo la kumuabisha

Usifikir ulikuwa n wakati mwepes kwa Yusufu uwe na uhakika alikuwa na mawazo na wakati mgumu Sana lakini alifanya maamuzi kiroho
No wonder Mungu aliamua kuptisha kusudi la kuukomboa ulimwengu mikononi mwa Yusufu

Jambo lingine utakaloliona Ni kwamba Yusufu alianza alifanya uamuzi wa kufikiri Nina uhakika kabisa aliingia kuomba hekima mbele za Mungu kujua Nini afanye juu ya usaliti huu wa mchumba wake!!!!

Hili linanipa kabisa kuona Namna Yusufu alivyokuwa anafasir Mambo kiroho na kumsaidia kutembea kwenye mapenzi ya Mungu!!!

Matayo:1.20
Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

Utagundua Kwamba kufikiri kwake hakukuwa kufikir kwa kawaida alikuwa anafikri huku anaomba maongozi ya Roho Mtakatifu juu ya Nini afanye juu ya Mariam
Kwann ninasema hivi kwa Sababu Malaika alipomjia Ndotoni akamwambia asihofu kumchukua 

Hili linanipa uhakika ya kwambaa alikuwa anajiuliza Kama amchukue na mimba asiyojua n ya Nani au asimchukue!!!!!

Malaika aalileta majibu ya maombi hayo

Sasa Jambo lingine utakaloliona hapa Ni mfumo wa  ujio wa ujumbe serious Kia's hiki Kuja kwa Yusufu
Kumbuka majibu ya maombi hayo yalikuwa n majibu yanayobeba wokovu wa ulimwengu wote

Kumbuka hapa n swala la kuzaliwa kwa Yesu mwokozi wa ulimwengu

Kilichonipa shida kuelewa n kuona Majibu ya Maombi hayo yanakuja kupitia ndoto

Nilitegemea Mungu azungumze naye kwa malaika live au yeye mwenyewe lakin alikuja Ndotoni
Nikafikir ndoto ambazo zimekuwa zikipita ndani mwangu na uzito ambao huwa ninazipa nikagundua Kuna Mambo mengi Sana ambayo sikuwa serious nayo

Kumbuka utii wa Yusufu juu ya ndoto uliokoa maisha ulimwengu mzima
Kuzaliwa kwa Yesu
Tazama namm hapa

Ayubu:33.14
Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.
 
Ayubu:33.15
Katika ndoto katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;

Ukisoma hapa utagundua kabisa Mungu huwa anasema na mioyo ya watu kupitia ndoto ila Ni wachache Sana wanaofasr kiroho ndoto wanazoziota!!!!

Nlipogundua hili binafsi nilianza kuandika Kila ndoto ninayoota na kuanza kutafuta maana yake na ujumbe uliomo ndani mwake

Nimeona matunda yake

Wewe unapoota huwa unalichuliaje swala la ndoto ???

Pengine ungetii ndoto uliyoota ungekuwa umepiga hatua kubwa Sana Katika maisha yako kiroho, kiuchumi nk nk

Jizoeze kufasir Mambo kiroho kwa sababu kuna Siri kubwa ndani mwake
MUNGU AKUBARIKI