Kwanini ninasema hivi
Kwa sababu nimekuja kugundua kwamba Kuna Mambo mengi Sana amabyo Mungu hutaman yatufukie kwa wakati lakini huwa inakuwa vigumu sisi kuchukulia uzito kwa sababu tunatembea Sana na mitazamo ya kibanadamu kuliko tunavyotafsir kiroho
Kuna Mambo ukiyatazama kwa namna ya kawaida huwezi kuona mpango madhubuti wa Mungu ndani yake
Umewahi kujiuliza kwann Paulo alikaza Sana kuombea kanisa la Efeso juu wao kuwa na namna ya kiungu ya kutazama mambo!!!
Waefeso:1.18
macho ya mioyo yenu yatiwe nuru mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;
Ukitazama kwa makini Utaona kabisa msisitzo wa Paulo upo kwenye uwezo wa mioyo yao kuona
Kumbuka kuona kwamba moyo Ni pamoja na Namna mtu anavyo uafasr Mambo anayokutana nayo Kila siku
Anasema macho yatiwe nuru(yapewe uwezo/power) to see in Godly way the things of our everyday lives
Kwann macho yatiwe nuru(ya kiungu)
Tazama maneno haya
1 Wakorinto:2.14
Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni
Maana yake nn
Tafsr Yake n kwamba kuna vitu vingi Sana Mungu huwa anavipitisha kwenye maisha Yetu ya Kila siku na tunayaona kwa jicho la asili(kibinadamu) na kwa sababu hiyo tunakosa uwezo wa kuona kitu au faida za kiroho(kiungu) zilizomo ndani mwake
Nataman nikitazamishe Mambo kadhaa kwenye maandiko uyaona kwa undani
2 Wakorinto:4.4
ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.
Ukitazama tofauti ya mtu mwamini na mtu asiyemwamini n utendaj Kaz wao wa utu wa ndanj
Kuna mmoja ana Fikra zinazoona Kiroho Kuna mwingine ana upofu hawez kuona Kiroho
Maana yake n kwamba katika uhalisia wa kiungu haoni chochote anaona uhalisia wa Jambo hilo kimwili ambalo kwa kweli Lina uhalisia mkubwa Zaid Kiroho kuliko mwilin anakoona yeye
Ngoja nkupe mfano
Bila Shaka umewah kusoma habr za kuzaliwa kwake mwokozi(Yesu) katika kitabu Cha Mathayo
Ngoja tutazame kwa pamoja
Utaona kabisa Yusufu na marina walikuwa kwenye hatua ya uchumba
Lakin Cha ajabu Mariam alikuwa tyr ana mimba ambayo kimsingi sisi tunajua kabisa n matokeo ya Roho mtakatifu kuja kutimiza kusudi maalumu
Na Jambo lilinishangaza Ni kuona Namna Yusufu alivyo fanya maamuzi juu ya mimba aliyoiona kwa mchumba wake na kwa kweli haikuwa ya kwake na hakujua n ya nan
Maandiko yanasema akaazimu moyoni mwake kumwacha kwa Siri
Kwann kwa sababu alikuwa mtu mwenye haki(mtu wa kiroho) Kia's ambacho pamoja na kwamba mchumba wake ameamua kumasaliti lakini hakutaka kufanya liwe Jambo la kumuabisha
Usifikir ulikuwa n wakati mwepes kwa Yusufu uwe na uhakika alikuwa na mawazo na wakati mgumu Sana lakini alifanya maamuzi kiroho
No wonder Mungu aliamua kuptisha kusudi la kuukomboa ulimwengu mikononi mwa Yusufu
Jambo lingine utakaloliona Ni kwamba Yusufu alianza alifanya uamuzi wa kufikiri Nina uhakika kabisa aliingia kuomba hekima mbele za Mungu kujua Nini afanye juu ya usaliti huu wa mchumba wake!!!!
Hili linanipa kabisa kuona Namna Yusufu alivyokuwa anafasir Mambo kiroho na kumsaidia kutembea kwenye mapenzi ya Mungu!!!
Matayo:1.20
Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Utagundua Kwamba kufikiri kwake hakukuwa kufikir kwa kawaida alikuwa anafikri huku anaomba maongozi ya Roho Mtakatifu juu ya Nini afanye juu ya Mariam
Kwann ninasema hivi kwa Sababu Malaika alipomjia Ndotoni akamwambia asihofu kumchukua
Hili linanipa uhakika ya kwambaa alikuwa anajiuliza Kama amchukue na mimba asiyojua n ya Nani au asimchukue!!!!!
Malaika aalileta majibu ya maombi hayo
Sasa Jambo lingine utakaloliona hapa Ni mfumo wa ujio wa ujumbe serious Kia's hiki Kuja kwa Yusufu
Kumbuka majibu ya maombi hayo yalikuwa n majibu yanayobeba wokovu wa ulimwengu wote
Kumbuka hapa n swala la kuzaliwa kwa Yesu mwokozi wa ulimwengu
Kilichonipa shida kuelewa n kuona Majibu ya Maombi hayo yanakuja kupitia ndoto
Nilitegemea Mungu azungumze naye kwa malaika live au yeye mwenyewe lakin alikuja Ndotoni
Nikafikir ndoto ambazo zimekuwa zikipita ndani mwangu na uzito ambao huwa ninazipa nikagundua Kuna Mambo mengi Sana ambayo sikuwa serious nayo
Kumbuka utii wa Yusufu juu ya ndoto uliokoa maisha ulimwengu mzima
Kuzaliwa kwa Yesu
Tazama namm hapa
Ayubu:33.14
Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.
Ayubu:33.15
Katika ndoto katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;
Ukisoma hapa utagundua kabisa Mungu huwa anasema na mioyo ya watu kupitia ndoto ila Ni wachache Sana wanaofasr kiroho ndoto wanazoziota!!!!
Nlipogundua hili binafsi nilianza kuandika Kila ndoto ninayoota na kuanza kutafuta maana yake na ujumbe uliomo ndani mwake
Nimeona matunda yake
Wewe unapoota huwa unalichuliaje swala la ndoto ???
Pengine ungetii ndoto uliyoota ungekuwa umepiga hatua kubwa Sana Katika maisha yako kiroho, kiuchumi nk nk
Jizoeze kufasir Mambo kiroho kwa sababu kuna Siri kubwa ndani mwake
MUNGU AKUBARIKI
No comments:
Post a Comment