Popular Posts

Saturday, November 9, 2019

KWA NINI MUNGU ANATAKA TUENENDE KWA ROHO?


Sehemu ya 2

....... Tuendelee tulipoishia

➡ Tuliona sababu kadhaa za Kwann Mungu anataka tuenende kwa Roho

➡Sababu inayofuata

2⃣ ili atusidie kuomba yale tunayotakiwa kuyaomba kwa wakati huo

📖Warumi 8:26
kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua   kusikoweza kutamkwa

➡ Tafsiri yake ni kwamba kuomba sio tatzo

➡ Unaweza ukaomba na ukaomba vbaya

➡ Au isivyokupasa

➡ Sasa kuendenda kwa Roho inakupa upako wa kufanya Maombi ambayo Mungu akiyasikia anakuwa na priority namba moja kuyajibu

➡ ```Udhaifu unaozumgumziwa ni wa namna  mbili
moja si rahisi kwa jinsi  ya  mwili kuomba kwa muda mrefu kwa sababu mwili ni dhaifu na
pili udhaifu tulionao ni kushindwa kuomba jinsi inavyotupasa kuomba.
```
➡ Ma hapa tunatakiwa kujiuliza swali namna ipi tunatakiwa kuomba kwa usahihi/Au itupasavy0 Ni kivipi

➡ Sasa  tunapoongozwa na Roho, maana yake moja anatusidia tuweze kuomba na zaidi anatufundisha namna ya kuomba  na kutuongoza  yapi tuyaombee kwa wakati huo  au kipindi hicho

➡ Mfano wewe unaweza ukawa unaomba upako wa Roho Mtakatifu katika huduma na yeye  Roho Mtakatifu, anajua kwamba  ameshakutia mafuta  na shida uliyonayo ni kutokujua namna ya kushirikiana na upako wake ulio juu yako. Hivyo yeye atakuongoza kuomba kwa habari ya kushirikiana  na upako aliouweka juu yako. Kwa  kifupi yeye kwa sababu ndiye mwenye maisha yako atakuongoza siku zote kuomba yale unayotakiwa kuyaomba kwa majira hayo iwe kuhusu masomo, ndoa, kanisa, nchi n.k.

3⃣ ili atuongoze katika kufanya maamuzi sahihi juu ya Maisha yako

📖 2Wakorinto 3:17
Basi Bwana ndiye Roho, walakini alipo Roho  wa Bwana, hapo ndipo penye  uhuru

➡ Uhuru wa nin Uhuru wa kimaamuzi unakuwa na free mind

➡ *Undirstubled mindset*  unakuwa unaamua huku ukiwa unatambua matokeo ya ulichokiamua

➡ Hauamui kwa sababu ya pressure yoyote,,si kwa sababu uingne eyote mbali na muongozo wa Roho kuamua uamuavyo

➡ pia ukisoma warumi 8:1-2 inasema 
*sasa, basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu, kwa sababu sheria ya Roho wa uzima  ule ulio katika kristo Yesu imeniacha huru, mbali  na sheria ya dhambi na mauti*
  kwako

➡ kufanya maamuzi ni sehemu  ya maisha ya mwanadamu
Yapo  maamuzi  mengi sana  ambayo mwanadamu anatakiwa kufanya na hawezi kukwepa kuyafanya

➡ Sasa Mungu kwa kulijua  hilo ametupatia Roho Mtakatifu ili atusaidie katika kufanya  maamuzi

➡ Roho Mtakatifu anapokuwa Bwana   kwako, yaani  mtawala, kiongozi ndipo anapokupa uhuru juu ya kufanya maamuzi katika maisha yako

➡ Maana yake ulikuwa hujui nifanye nini? Niamueje ? Sasa yeye anakuletea uhuru ndani wa  kufanya jambo ambalo anajua ni la mafaniko  kwako
Kumbuka siku zote nia ya Roho ni uzima na amani

➡*```Huenda ziko sababu nyingi ni kwa nini unatakiwa uenende  kwa Roho, lakini hizi tatu ndizo Mungu alizonipa tuweze kushirikiana kujifunza. Ni imani yangu kwamba utakapoamua kutaka na kupenda kuongozwa na Roho ndipo utakapoona Mungu akijifunua```*

Ubarikiwe kwa kufwatilia somo 🙏🏿

KWA NINI MUNGU ANATAKA TUENENDE KWA ROHO?

Sehemu ya 1⃣

➡Ni wazi kabisa ya kuwa Mungu ako na mpango madhubuti na kila mwamini na Kuna mambo ambayo anataman yatokee maishan mwetu

➡Na moja ya mikakati aliyoiweka n kutupa namna tunavyotakiwa kuishi yaani kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu

➡ Tazama  maandiko haya

➡ Ukisoma katika warumi 8:14 Biblia inasema
kwa kuwa wote wanaoongozwa  na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu
na pia Paulo kwa wagalatia anasema Basi nasema Enendeni kwa Roho,wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili Wagalatia  5:16.

➡ Anapotaka tuongozwe na Roho Mtakatifu anajua Kuna faida tutapata

➡Vinginevyo Kuna ugumu tutakutana nao mbele ya safar

📖 Wafilipi:1.6
```Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;
```
➡ Usitake Mungu atembee nawewe wakat uko na shida ikiwa wakat haukuwa na haja hukutaka kutembea nae ni kosa

➡ Usitake Mungu amalize mwendo nawewe wakati hakuaanza nawewe ni kosa

➡ Hapa tunaona jinsi Paulo anavyosisitiza kwa makanisa ya Rumi na korinto kuhusu suala zima la kuongozwa  na Roho  Mtakatifu. Anawaambia warumi kwa  kuwa wote wanaongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana  wa Mungu maana yake haijalishi  ana umri gani, ni wa dhehebu gani, jinsia gani maadamu anaongozwa  na Roho wa Mungu huyo ni mwana wa Mungu na bado anawaagiza wagalatia akisema Basi nasema  enendeni   kwa Roho………….. anaposema enendeni maana  yake  mkiongozwa  na Roho, au mkimfuata  Roho katika yale anayowaagiza.

➡Kwa tafsiri hiyo swala la kuenenda kwa Roho sio la kiongoz wako wa fellowship, mchungaji, bishop, chair

➡ No ni la kila mwamini ndani ya kanisa
➡Ni la kwako

➡ Na hatuongozwi tu tunapotaka kububiri tunapotaka kufundsha , ni Zaid ya hapo

➡ Ni swala ambalo linatakiwa kuwa mfumo halis wa maisha yako ya kila siku

➡ hata vitu vdgo vdgo ambavyo unafikiri havihitaji muongozo tafuta muongozo

➡ Anaposema enenda maana Yake utembee kwa kufuata malekezo

➡ Unataka kuoa muulze yeye unataka kusomea nn muulze yeye unataka kuacha iyo Kaz muulze yeye

➡ Anajua unachotakiwa kufanya kuliko unavyotaka na kutarajia kufanya

➡ zipo sababu za msingi  kwa nini tunatakiwa kuongozwa  na Roho  sasa hapa sizungumzii kazi za Roho mtakatifu najua zipo kazi nyingi anazozifanya Roho Mtakatifu lakini mimi nazumgumzia sababu za kuongozwa  na Roho Mtakatifu, ambaye ndio agano jipya la Mungu kwetu

📖Tazama  yeremia 31:31
➡ katika hiyo Yeremia Neno linasema
Angalia siku zinakuja asema Bwana nitakapofanya  agano jipya na nyumba ya Israel....
Sasa ukiendelea kusoma mistari inayofuata utaona anazungumzia habari za *kutia sheria yake katika mioyo ya watu*

➡ Sasa hili ndilo agano jipya la Mungu pamoja na wanadamu
Sasa usipojua kwa nini unatakiwa kuongozwa na Roho na siyo akili zako, au mazoea, au taratibu za kwako n.k. hautajua umuhimu wa kuongozwa na Roho Mtakatifu
na pili hautaona sababu za kuongoza na Roho Mtakatifu

➡lengo la ujumbe huu ni kukufundisha sababu za msingi  za kwa nini unatakiwa kuongozwa na Roho Mtakatifu
na siyo akili  zako au mawazo yako
```Sasa  tuangalie sababu hizo za msingi```

➡ Moja,,,,ili  tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu na kuyapokea mambo ya Roho na Mungu.

➡Iwakorintho 2:12 inasema Lakini sisi hatukupokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, *makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa  na Mungu*

➡ na ule wa 14 unasema
Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei  mambo ya Roho wa Mungu maana kwake huyo ni upuuzi, wala *hawezi kuyafahamu kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya Rohoni* . Unapoongozwa  na Roho Mtakatifu ndipo anapokusaidia kujijua wewe mwenyewe vizuri.

➡Anaposema  upate kuyajua yale ambayo Mungu amekupa katika maisha yako Ana maanisha maisha yako

➡ Juzi nmekueleza Kuna watu hawajui wanataka nn maishan mwao hawajui wafanye nn na maisha yao

➡Roho Mtakatifu anapokuja ndani yako anaanza kukupa elimu ya kufunuliwa kwako binafsi unaanza kujilewa

➡ Kuna watu hawajiheshimu kwa sababu ambazo hata wao hawazijui
➡ Kuna mtu anaona hawez kufanya maamuzi sahh bila ya fulan na hajui kwann yupo ivo

➡ ```Nakuombea Sasa katika jina la Yesu uanze kuweza kufanya maamuzi bila ya fulan```

➡ Huo n udhaifu

➡ Anapoamza Roho Mtakatifu kukuongoza ukaenenda kwa Roho my God my Lord maamuzi yako yatakuwa yanashangaza wengi

➡ Roho mtakatifu atakusaidia kujua aina ya vipawa  ulivyonavyo, karama za Rohoni ulizonazo, huduma ulizonazo kama umeitwa huko, atakusaidia kujua vizuri unaweza kufanya  nini na nini  huwezi, kipi ufanye  na kipi usifanye, atakusaidia kujua baraka zako za kiroho  na kimwili pia

➡ Infact anakusidia kulijua kusudi   la Mungu katika maisha yako

➡Anakujuza n vipi ufanye ili uweze kulifikia hilo kusudi na zaidi  atakupa upako/ nguvu za kuweza kuyapokea yale yote anayo kuagiza ili uweze kulifikia kusudi lake kwako na kuzirithi baraka zako

➡ Angalia  kitabu hiki Cha zaburi

📖katika zaburi 32:8  anasema *“Nitakufundisha  na kukuonyesha njia utakayoienda nitakushauri, Jicho langu likikutazama*

➡ Binafsi nataka jicho lake linitazame linipime mienendo yangu ya kila siku

➡Nataka anionyeshe njia ya kuiendea nataka anishauri

➡ Kwa le0 naomba tuishie hapa tutaendelea wakati ujao