Popular Posts

Tuesday, February 11, 2020

JIZOEZE KUOMBA ROHO YA HEKIMA NA UFUNUO KATIKA KUMJUA MUNGU

Elikado Mwasenga

Karibu tujifunze pamoja neno la Mungu juu ya Maombi haya yakitofauti
Bwana Yesu asifiwe SANa!

Waefeso 1:17-18
Waefeso:1.17
Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye

Waefeso:1.18
macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue....

Ukitazama kwa makini maandiko haya utaona Kuna mambo kadhaa Paulo alikuwa anamuomba Mungu juu ya Kanisa la Efeso
Na swali la muhimu kujiuliza Ni kutaka kujua kwanini alikuwa anawaombea wapate Roho ya namna hii?

2 Petro:1.2
Neema na iwe kwenu na amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu

2 Petro:1.3
Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.

Nataka nkutazamishe kitu
Kuna namna utagundua kuwa na Roho Mtakatifu Ni jambo moja lakin Roho Mtakatifu kuOperate kama roho ya ufunuo na ya hekima Ni jambo lingine

Sababu kadhaa za kwanini Paulo alikuwa analiombea Kanisa la Efeso Maombi ya Aina hii

1. Wamjue Mungu kwa maarifa ya mapenzi yake
Yaaani kumjua Mungu kwa kadri anavyotutaka tumjue

Wakolosai:1.9
Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni

Angalia maandiko haya utagundua kwamba Paulo aliwahi liombea pia kanisa la kolosai wapate maarifa ambayo Ni mapenzi ya MUNGU kwao

2. Wawe na ufahamu wa rohoni utakao wasaidia kutembea na jicho la Kimungu juu ya eneo walilopo na kwa kila hatua wanayopitia
Kumbuka kimaandiko Kuna maneno ya rohoni na Kuna maneno ya mwilini

1 Wakorinto:2.12
Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu

1 Wakorinto:2.13
Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni

maanA yake Nini ni kwamba Roho Mtakatifu yupo ndani ya kila Mtu aliyemwamini Yesu siko alipokuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako lakini swala la hekima na UFUNUO Ni juu ya wewe kukaa na kujifunza kwake

Kumbuka anachotusemesha hapA Ni kwamba anasema anatufundisha kwa maneno ya rohoni!
Yaani Ni kwamba Kuna weza kuwa na Jambo la mwilini lakni kwa jicho la mbinguni Kuna tafsir ya kiroho na hutolewa kwa maneno ya kiroho

Sababu ya tatu 

3. Ili kujua mambo ambayo Mungu amewaandalia Kama watoto wake  (1Wakorinto 2:9-10)

Katika fungu hili Biblia
1 Wakorinto:2.9
lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao

1 Wakorinto:2.10
Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu

Ukitazama kwa makini utagundua kwamba Kuna namna tunaweza kuwa ndani ya Yesu na bado tusipate faida ya kuwepo ndani mwake

Kwa sababu hiyo tunajukumu la kukaa chini kuanza kuzijua Siri za ufalme

Na Kuna Mambo mengi sana ambayo MUNGU amewawekea watu maalumu watu awapendao
Na namna ya kuyapata Ni kuwa na ufunuo wa Roho

Kuna kiwango Cha maisha hutakifikia bila HEKIMA hii na UFUNUO huu

Na hekima hi ipo kwenye Angle tofaut tofauti
Unaweza kuwa muimbaji, mhubiri, mfanya biashara, baba, mama nk nk
Maadamu tu upo hapA duniani unahitaji hii hekima
Unahitaji huu UFUNUO

Nataka upate ufahamu kwamba kwamba Kuna baadhi ya maeneo kwenye maisha yetu ya kila siku hatutavuka Kama hatuna Hekima na Ufunuo huu!!!!!

Maisha yako Ni matokeo ya ufunuo ulioubeba

Kazi ya roho ya ufunuo ni kumfunua Mungu kwa kiwango ambacho bado hujakiona wala kukizoea ili kuboresha uhusiano wako na Mungu na kukufanya umaanishe katika kumpenda yeye

```kazi ya roho ya hekima ni kukupa ufahamu (maarifa), werevu na busara katika kufanya maamuzi sahihi kuhusu uhusiano wako na Mungu na maisha yako kwa ujumla```

Kumbuka hilo Ni mhimu Sana ukaelewa hivyo
Kumbuka MUNGU Ana mpango mzuri Sana na maisha yako
Anataka uwe mtu mkuu

Katika ufunuo kuna mambo ambayo Mungu atayaleta kwako na yanahitaji hekima katika kuyafasiri kuyanena na kutenda

Unahitaji hekima unahitaji Ufunuo
Jambo baya zaidi Ni kwamba
 
shetani atakuruhusu uombe MAOMBI ya Vita lakni akakufanya usione umuhimu wa kuhitaji hekima na ufunuo
Utaomba muujiza na uponyaji akni hekima na Ufunuo hautaona Kama Ni Jambo la maanA kwako
Lakin yote tunahitaji yamo ndani ya hili la hekima na ufunuo

JIZOEZE KUOMBA ROHO YA HEKIMA NA UFUNUO

Maana yangu Ni kwamba weka utaratibu wa kuomba juu ya hili mara kwa mara
Toa sadaka msemeshe Mungu mwambie nataka kukujua
Funga omba kwake mwambie nataka kukujua

JIZOEZE KUOMBA ROHO YA HEKIMA NA UFUNUO

Ukitembea na tabia hii ghafla utanza kuona Mungu anaanza muwa halisi kwako maisha yako hayatakuwa Mzigo yatakuwa baraka!