➡Namshukuru Mungu kwa kunipa kibari cha kutumika katika madhabahu hii
Mungu akuhudumie vile alivyokusudia
➡ Tukisoma kitabu cha Yohana Sura ya 4 na mstari ule wa 23 hadi 24
📖 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
Yohana 4 :23
📖Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Yohana 4 :24
➡ Katika mstari wa 23 tunaona Yesu alipokuwa akizungumza juu ya wakati na majira yatakayofika katika maisha ya watu yatakayowapasa watu kufikia katika hatua ya kumuabudu Mungu katika *Roho na Kweli*
,➡ Na kwa tasfiri hii inatufahamisha kuwa kama kuna kuna kumwabudu Mungu kuliko katika Roho na *kweli*(halisi) basi kuna namna nyingine ya kumuabudu Mungu kusiko katika Roho na *Kweli( *halisi* ) yaani kusiko halisi
➡ Na tunaona Yesu akizungumza zaidi kuwa hayo majira ambayo anayazungumzia ya kuwa yamekwisha kuja sasa yapo maana yake haya majira ninayozungumza na wewe ndio majira ambayo Kristo alikuwa akiyazungumzia katika kitabu cha yohana
➡ Haya ndio majira ambaya yanatupasa kumwabudu Mungu katika *Uhalisi* (roho na kweli) hakuna majira tunayoyatarajia zaidi ya haya
Usije ukafikiri kuwa kuna majira mengine zaidi ya haya
➡ Kwa hiyo Yesu alipokuwa anasema kuwa katika majira jayo itawapasa waabuduo kumwabudu Mungu katika *Uhalisi* ( roho na kweli)
Maana yake kuna namna fulani ambayo ilitumika katika kumwabudu Mungu ambako siko *halisi*
➡ Kumwabudu Mungu katika roho na kweli(halisi)
Unakuwa na mfumo fulani wa maisha ambayo Mungu anataka uwe au unakuwa na maisha ya kumpendeza na maisha yampendezayo Mungu ni yale yalio katika mapenzi yake
➡ Kwa hiyo kumwabudu Mungu kama apendavyo yeye huko ndiko kuabudu kuliko halisi
➡ Kwa hiyo ili uweze kumwambudu Mungu katika roho na kweli( *halisi* ) lazima utafuta kwanza kujua kuwa kumwambudu Mungu kuliko halisi kukoje
➡ Katika mstari huu biblia inatuambia juu ya kumuabudu Mungu katika roho na kweli yaani kuliko halisi
✍ hauwezi kumwabudu Mungu katika roho na kweli kama hautajua iyo namna ya kweli ikoje,
Hautaweza kumwabudu Mungu katika Uharisi kama hautajua uhalisi huo ni upi
➡ Kumbuka hapa mwanzo nimesema kuwa *Mapenzi ya Mungu ndio uhalisi wenyewe*
➡ Yaan uweze kufahamu huo uhalisi wenyewe ukoje
➡ Lakini pia ukiangalia katika ule mstari wa 23
Biblia inatuambia kuwa Mungu anawatafuta watu kama hao wamuabudu
➡ Ko ili uweze kufikia katika hatua ya kumuabudu Mungu katika uhalisi( roho na kweli) *ni Muhimu kwanza uyajue mapenzi ya Mungu juu yako*
➡ Kumbuka somo letu ni juu ya kuyajua mapenzi ya Mungu juu ya kuumbwa kwako
➡ Ko haya ni majira ambayo Mungu anatamani kuwaona watoto wake(watu wake ) wakifika katika hatua ya Kumuabudu yeye katika Mapenzi yake
➡Mungu anatamani tuyafahamu mapenzi yake juu ya maisha yetu ili itusaidie kumuabudu katika roho na kweli
➡Mungu anatamani kuwaona watu wake wakiishi katika viwango ambavyo alivikusudia katika maisha yao
➡ Ukiyajua mapenzi ya Mungu itakusaidia kumuabudu katika uhalisia anaouhitaji
➡ Kwa nini Mungu aliruhusu wewe uzaliwe wakati kuna wengine mimba zao ziliaribika tangu wakiwa tumboni mwa mama zao
➡ Na wengine baada ya kuzaliwa tu hawakupata nafasi ya kuishi kama ulivyoishi wewe hata siku ya leo
➡ Na pengine wewe umezaliwa ukiwa na ulemavu na wengine wamezaliwa wakiwa na viungo vyote!
➡Na pengine umezaliwa na viungo vyote na wakati huo huo tena yawezekana katika kipindi hicho hicho na mahali hapo hapo kuna wengine wamezaliwa wakiwa na upungufu
➡ Kwa nini Mungu aliruhusu uzaliwe hivyo ulivyo haijarishi ni nanma gani uko lakini kwa nini Mungu ameruhusu uwe hivyo
➡ Kwa nini Mungu ameruhusu uzaliwe na uishi katika hilo eneo ambalo upo
Kwanini Mungu ameruhusu uwe mtanzania kwa nini usiwe mchina? Na wengineo ukazaliwe katika maeneo mengine?
➡ Haya ni maswali ambayo natamani uyaweke katika ufahamu wako na uendelee kujiuliza wakati tunaendelea na somo hili
➡ Kwa hiyo ukiwa na maswali ya namna hiyo katika ufahamu wako itakutengenezea kiu ya kutaka kujijua wewe ni nani na ni nini mapenzi ya ya Mungu juu ya maisha yako
➡ Kwa nini Mungu alikuumba wewe kwa namna hiyo ni nini sababu ya kuubwa kwako???
➡ Mungu hawezi akakufunulia hayo kama wewe hautakuwa na kiu na shauku ya kutaka kuyajua
➡ Tukisoma katika kitabu cha mwanzo sura ya kwanza kuanzia mstari wa kwanza tunaona Mungu namna alivyokuwa katika uumbaji wake aliumba vitu vingi kwa neno lake na vikawa alitamka Anga
,Nuru ,wanyama,mimea,ndege,na vitu vingi sana alivyoweza kuvitamka na vikawa kama alivyotamka
➡ Ngoja nikupitishe mahala fulani
➡ baada ya vile vitu Mungu alitamka kutokea kwa namna ambayo Mungu aliitamka tunaona Mungu akaingi katika hatua ya kumuumba mwanadamu
➡ Angalia kitu kilichoendelea hapo
➡tunaona Mungu alipofika katika hatua ya kumuumba mwanadamu biblia haituambii kwamba Mungu alimtamka mwanadamu
➡ *Kwamba Mungu akasema na awe mwanadamu na akawa* hapana bali Biblia inatuambia kwamba Mungu alipofika katika hatua hiyo kwanza aliitisha kikao cha halmashauri yake
➡ Na kuwasilisha mpango wake Na akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu na kwasura yetu
➡ Ebu tusome maandiko kidogo
📖: Mungu akasema, Na *tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu;* wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Mwanzo 1 :26
➡ Na tukisoma katika sura ya pili na ule mstari wa saba
📖 *Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.*
Mwanzo 2 :7
➡ Tunaambiwa kuwa Mungu alimfanya Mtu maana yake kulikuwa na kaprocess fulani katika uumbaji wa mwanadamu ambako hakakufanya katika uumbaji wa kitu chochote
➡Maana yake Mungu alitafuta mahali penye udongo mzuri , akaufanya kuwa mbichi,akamuundia huyo mtu mwili utakao mbeba ,akapulizia pumzi ikawa nafsi hai kisha akamuweka huyo mtu aliyefanana naye
: ✍ *Kumbuka mwili wako sio wewe bali mwili ni chombo kilichokubeba wewe*
➡Ko tunapokuzungumzia wewe hatuuzungumzii mwili wako ndio maana mtu akifa tunasema fulani katutoka japo mwili wake tunakuwa nao
Mfano raisi wa kwanza wa taifa la tanzania tunasema amekufa na tunamuadhimisha kila mwaka lakini mwili wake tunao mpaka leo
➡ Nimekupitisha hapo ili uone jinsi ulivyowathamani kubwa sana isiyoweza kukaribiwa na kitu chochote duniani
➡ nini maana ya maneno haya maana yake Mwanadamu alikuwa na nafasi/thamani kubwa kuliko kitu chochote ambacho Mungu alikifanya katika ulimwengu uliopita ,uliopo na hata ujao hakuna kitu chochote kitakachofikia thamani ya mwanadamu
✍kabla Mungu hajamuumba mwanadamu alipokuwa akilitoa wazo lake juu ya uumbaji wa mwanadamu tunaona kulikuwa na sababu iliyomfanya Mungu amuumbe mwanadamu
➡ Baada ya Mungu kuumba ulimwengo na vitu vyake na kuona kuwa ni vyema
Ndipo likatokea wazo la kuumbwa kwa Adam
📖 Mungu akasema, Na *tumfany:e mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu;* *wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa* *kitambaacho juu ya nchi* .
Mwanzo 1 :26
➡: Kwa hiyo kumbe mwanadam aliumbwa na kupewa jukumu la kusimamia kila kitu ambacho Mungu alikiumba
➡: Katika huu mstari tunaona Mungu anapsema tumfanye mtu ameambatanisha na majukumu ya huyu mtu anayetaka kumuumba
➡ Kwa hiyo kumbe tunaona mwanadamu kuwa aliubwa kwa makusudi maarumu ya Mungu
➡: Kwa hiyo katika kila maisha ya mwanadamu yeyote kuna makusudi ya Mungu juu ya uumbaji wake
➡: katika sura ile ya kwanza kitabu cha mwanzo mstari ule wa mwisho tunaona kuwa Baada ya Mungu kufanya kila kitu na kumfanya huyo mwanadamu na kutoa amri ya kuzaliwa kwa mwanadamu mwingine
Biblia yangu inaniambia kuwa Mungu aliona ni vyema
📖 *Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.*
Mwanzo 1 :31
➡: Mungu aliona vema kumuumba mwanadamu
Hata leo bado Mungu anaonavema kukufanya wewe
➡: Mungu anaona vema kuumba wewe kaka
Mungu anaonavema kukuumba vema wewe Dada
➡: Mungu anaona vema kukuruhusu uzaliwe katika familia hiyo ,Mungu anaona vema uzaliwe katika hiyo jamii,eneo/mkoa na wilaya uliyezaliwa
*Ooh halehuyaaa*
➡: Sisi ni wanadamu na yeye ni Mungu ni mkuu sana hajawai kosea hata kidogo kwa hiyo Mungu kukufanya wewe hajakose mtumishi ameona ni vema
➡ Ni vema wewe kuwa binti
Ni vema wewe kuwa kijana wa kiume ni vema ni vema
➡ Mungu kukuruhusu aliona kuwa ni vema na aliona kuwa unafaa kabisa kuwa katika familia hiyo na mahali hapo ulipo
: 😢 Wako watu wanakaa na kumlaumu Mungu kwa kuruhusu wazaliwe katika familia hapana usimlaumu Mungu
➡ Unadhani kwa nini anaona vema
Kuna mapenzi / makusudi yake ndani ya maisha yako
➡ Sikiliza mtumishi Hiyo haimpi shida Mungu bado anamakusudi na wewe
Bado anamakusudi na wewe
➡ Haijalishi kuzaliwa kwako kulikuwaje
Yawezekana mimba yako ilipatikana kwenye uzinzi,
Yawezekana ilipatikana kwa waganga na mizimu ya mababu wa ukoo
➡ Mungu anakuhitaji anatamani uyafahamu mapenzi yake kwako ili aanze kuyatimiza
➡ Lakini pia wakati tunaendelea kujifuza somo hili la KUYAJUA MAPENZI YA MUNGU
➡Ni muhumu pia ukaweka maswali katika ufahamu wako
➡ Sasa tuendelee na sehemu nyingine tujifunze zaidi
➡ Kwa nini niyajue mapenzi ya Mungu?,
Kuna umuhimu gani wa mimi kuyajua mapenzi ya Mungu?,
Kitu gani kinatokea mtu akiyajua mapenzi ya Mungu?
➡ maswali haya yanaweza kukutengnezea au yakakuongezea shauku ya kutaka kujua zaidi
➡ Sikiliza mwana wa Mungu
📖Biblia inaposema *imewapasa* kumwabudu Baba katika Roho na kweli
➡Hili neno imewapasa maana yake hakuna namna ya kukwepa ni lazima ufanye hivyo
➡ Suala la kuyajua mapenzi ya Mungu katika maisha yako ni jambo la muhimu sana kuliko unavyofikri
➡ Na kwa sababu hatuwezi kumuabudu Mungu katika uhalisi kama hatuta yajua mapenzi yake kwetu basi Kuyajua mapenzi yake pia ni lazima sio ombi
➡ Sikiliza
Mungu kukuumba hivyo ulivyo hajakosea bwana ni sahihi kabisa haijalishi ni mazingira gani umezaliwa nayo
➡Kwa hiyo suala la kumuambudu Mungu katika roho na kweli sio ombi hauna chaguo la kupinga hapana ni lazima
➡ Yawezekana ulizaliwa katika familia ya machifu
Pia yawezekana ulizaliwa katiaka familia ya waabudu mizimu au yawezekana ulizaliwa katika familia ya kimasikini
➡ Kuna Ka usemi mmoja wanasema hivi kuzaliwa masikini sio shida ila ni tatizo kufa masikini
➡ Hiyo haimzuii Mungu kufanya yakwake
➡ Yawezekana Mungu alikuweka katika jamii yenye watu waliojaa shida na matatizo mbali mbali ili wewe ndi uwe mtatuzi wa matatizo yao lakin kwa sababu haujui nawew una ungananao kulala mika
➡ Uanze kuona na kutembea katika viwango ambavyo Mungu amekusudia juu ya maisha yako
➡ *Aiseeh ufahamu wako ufunguke siku ya leo kwa jina la Yesu Kristo*
➡ Kwa hiyo kila mwanadamu hajazaliwa kwa bahati mbaya yapo mapenzi ya Mungu juu ya maisha yako
➡ Lakini kama ungetambua mapenzi ya Mungu kwako ni yapi usingeishi maisha ya kawaida usingejichukulia kiwepesi wepesi
➡ Kuna watu wanaishi yaisha yasiyo yao sio ambayo Mungu alikusudia uyaishi ila kwa sababu haujui maisha yako halisi ni yapi umelidhika na maisha hayo
Umeridhika na hatua na viwango hivyo hivyo ulivyonavyo
➡Ungejiona kuwa ni mtu wa thamani sana katika dunia hii,katika familia yako,katika kikundi chako kanisani na maeneo mengine tena ungetamani kuwa ungewahi kuzaliwa
Wewe 👉
➡ Lakini kwa sabubu haujui unaona kama maisha unayoishi ndio ya kwako
Ati Mungu ndivyo alivyopanga
At maisha ndio haya haya
➡ Kama ungefahamu jinsi Mungu anavyokutarajia usingesema maneno haya katika kinywa chako
➡ *zinduka katika hivyo vifungo kwa jina la Yesu Kristo*
Na uyafahamu Mapenzi ya Mungu juu yako
➡ Sasa Utajiuliza *ninawezaje kufahamu Mapenzi ya Mungu kwangu*
➡: Sikiliza nikwambie Kitu mteule
➡ Ukitaka kujua vizuri kazi au maana sahihi ya kitu furani ni lazima kwanza umtafute yule aliyetengeneza hiyo kitu ndio akupe matumizi halisi ya hicho kitu
➡ Vivyo hivyo Wewe ni Mwana wa Mungu
Na Mungu ndiye muumbaji wako,ndie aliyekutengeneza wewe kwa hiyo yeye ndiye anayotafriri sahihi ya wewe.
➡ Nikitaka kujua kazi ya wewe ni lazima nimuulize aliyekutengeneza wewe ndio nipate kujua kazi na umuhimu wa wewe
➡ Kwa hiyo ili nijue mapenzi ya Mungu kwangu lazima niende nikamuulize Mungu mwenyewe ndiye aniambie kwa nini aliniumba ni nini sababu ya kuumbwa kwangu
➡ Kwa tafsiri hii Mungu ndiye anaye jua mapenzi yake kwako
Ndiye anayetua tafsiri sahihi ya kwako
➡ *We have to ask the lord who am i and what is my purpose*
➡ *What am borning for*
➡ *What am here for*
➡ Watu wengi tunaomba maombi mengi na magumu mbele za Mungu lakin tunasahau kuuliza Mungu *who am i* tusahau kumuomba Mungu kuwa atupe tafsiri sahihi ya maisha yetu
➡ Na kwa sababu haumulizi Mungu ili akuelezee wewe kwako shetani anatumia nafasi hii kupitisha watu katika maisha yako watakao kuelezea wewe tofauti watakaokupa tafrisi tofauti kabisa
➡ Yaan kama usipompa nafasi Mungu ya kukutafsiri wewe shetani anachukua nafasi hio kukutasfiri wewe tofauti na mapenzi ya Mungu
➡ kama hautajua wewe ni nani na ni nini makusudi ya wewe kuwepo shetani atakuletea tafsiri itakayokuelezea wewe tofauti na Mungu alivyotaka
➡Na anaweza akatumia watu wa karibu kabisa anaweza akawa mzazi wako au hata kiongozi wako wa kanisa kukuletea tafsiri tofauti
➡ Yawezekana Mungu kakuumbia Wewe katika Eneo la uchumi kuwa mwana uchumi mzuri utakayeisaidia jamii na kanisa lake
➡ Ila kwa sababu haujui Shetani anasogeza watu wenye tafsiri tofauti
➡Utasikia wakisema
wewe unaonekana una karama ya uchungaji au unaonekana kama mchungaji itabidi ukasomee uchungaji na inawezekana na kukusomesha wakakusomesha lakini kwa sababu haujui ni nini mapenzi ya Mungu kwako unaona ni kama Mungu ndio kawatuma kwako
➡Lakini kumbe ni tafsiri ya shetani kwako unajikuta unapoteza kusudi la Mungu kwako
➡Na haijalishi ni mambo gani unafanya au ni wapi unapita yawezekani ni mazuri kabisa lakin shida iko hapa je ni mapenzi ya Mungu kwako kwa wakati na majira hayo?
➡ Ni kweli ni muimbaji na unamtukuza Mungu katika uimbaji lakini je ni mapenzi ya Mungu wewe kuwa muimbaji
Ni kweli ni mchungaji na watu wanakupenda lakini je ni mapenzi ya Mungu wewe kuwa mchungaji
📖 *Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.*
1 Wakorintho 12 :7
*8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;*
1 Wakorintho 12 :8
*9 mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja* ;
1 Wakorintho 12 :9
*10 na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha* ;
1 Wakorintho 12 :10
*11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye* .
1 Wakorintho 12 :11
➡Kuna watu Mungu amewapa maarifa wengine hekima yatakayoweza kuisaidia jamii ,familia,na kanisa
➡Sisemi ni vibaya kuwa muimbaji hapana lakini je ni mapenzi ya Mungu Wewe kuwa?
➡Na kanisa linawategemea sana hawa watu lakini kwa sababu hatujui tumekimbilia katika maeneo mengine
Uchungaji,unabii,utume,uimbaji nk
➡Ni mapenzi ya Mungu wewe kuwa hapo ulipo
➡ Ni Muhimu sana kutafuta mapenzi ya Mungu kwanza katika kila jambo unalotaka kulifanya
➡Kabla haujafanya jambo ebu Muulize Mungu kuwa Je ni mapenzi yako Mungu mimi nifanye hili
➡Mungu alituumba ili tuishi katika maisha yake yaani mapenzi yake
➡Tafuta kuyajua Mapenzi ya Mungu kwako
Na ukijujua wewe ni nani itakusaidia pia kujua unatakiwa kufanya nini na kwa wakati gani Itakusaidia kujua kusudi la kuumbwa kwako
➡ Kuna vitu hautaruhusu vipite katika maisha yako
Kuna aina ya Mambo hautayafanya kabisa
Kwa sababu unajijua
📖 *ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu* .
2 Wakorintho 4 :4
➡Ni maombi yangu kuwa kila mahali ambapo ufahamu wako umefungwa ili usiweze kuelewa mapenzi ya Mungu kwako ukafunguliwe leo Kwa jina la Yesu Kristo
➡ Jitengenezee Mazingira ya kumuuliza Mungu kila siku
Kila hatua inayofuata katika maisha yako
➡Hakika Maisha yako hayawezi kuwa ya kawaida aisee
➡ Amen Mungu akubariki sana kwa kufuatana nami katika somo hili
➡Naamini kuna ufahamu umeupata siku ya leo
Unaoweza kukutoa katika hatua moja kwenda nyingine katika kumuabudu Mungu
➡: Ulikuwa nami
John Mwakyoma
Nawapenda nami
John Mwakyoma
Nawapenda