Popular Posts

Wednesday, July 3, 2019

JIFUNZE KUENENDA KWA ROHO ILI USIMHUZUNISHE ROHO MTAKATIFU

Bwana Yesu asifiwe
Si swala la unajickiaje au unataka Nn kutoka kwa Roho Mtakatifu Jambo la kwanza ndan ya ufahamu wako unatakiwa kutambua kwamba Roho Mtakatifu anaweza kuhuzunishwa na watu walibeba ndan Yao na gharama ya kumhuzunisha Roho Ni kubwa kuliko gharama ya kujifunza na kijitahid KUENENDA KWA ROHO ili usimhuzunishe,,,,

πŸ“– Waefeso:4.30
Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.

πŸ“– 1 Wathesalonike:5.19
Msimzimishe Roho;

Roho Mtakatifu ni Mungu, anayo nafsi ambapo ndani yake kuna hisia na kwa jinsi hiyo anaweza kufurahi au  kuhuzunishwa pia

♦ Kwa maana hiyo lazima tuwe Makini Sana na namna tunavyohusiana nae

Siku ulipokubali kumpa Bwana Yesu maisha yako kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako MUNGU alimuachilia Roho Mtakatifu aje kukaa ndani mwako na kukuongoza kwenye kila hatua ya maisha yako

Lakn mfumo wa kuish kwako lazima uzingatie vigezo na mashart ili Roho Mtakatifu asje akahuzunika na kukuacha

♦ Madhara ya kumhuzunisha Roho Ni mabaya kulko tunavyoweza kufikir kwa watu wa MUNGU na MUNGU pia lakn madhara anayoyapata mtu Ni makubwa kulko MUNGU kwa sababu MUNGU anajitolesheleza katka uungu wake na anasema mm ninawasamehe kwa ajili yangu mwenyew usje ukajidai ya kwamba wewe au Toba yako ndo sababu ya kusamehewa kwako

♦Kwa sababu ingekuwa sababu zipo mikonon mwetu Kuna watu tungepata shida sana kwa kuwa huwa hatuna misamiat mizur wakat wa kuomba huwa hatuna vifungu madhubuti wakat wa kutubu ashukuriwe MUNGU sababu za msamaha wa kila mmojA wetu zipo mikonon mwake mwenyewe

Haleluuyah,,,,,

Bwana Yesu asifiwe

kumuhuzunisha Roho Mtakatifu ni kumuwekea mpaka katika utendaji wake kwa kukataa uongozi, maonyo au ushauri wake  unaolenga kuwezesha utekelezwaji wa kusudi la Mungu kupitia mwanadamu

♦ Nataka nkutazamishe vitu ambavyo mtu akiviishi au kuvifanya huwa vinampa Roho Mtakatifu huzuni

Kuna mambo mengi sana juu ya hili eneo Lkn nataka nkutazamishe kwa uchache mwngine tutamalizia wakati ujao

 Wakati fulani nlkuwa nasoma kitabu Cha mtumishi wa MUNGU Benny Hinn,,,,, Anasema siku moja akiwa kuomba ghafla akaanza kupewa maono watu wanashuka wanazama kwenye ziwa la Moto alafu akatokea malaika akiwa na ujumbe wa MUNGU akasema hao unaowaona wanaangamia wanatakiwa watoke huko kupitia wewe

Alipo ona hayo akajaa uchungu ndani mwake akalia huku akishindwa kujizuia

♦ Hiii sio huzuni ninayo izungumzia

Huku kunaitwa kuugua kwa Roho Mtakatifu ndan yako sawa sawa na warumi 8:26

πŸ“– Warumi:8.26
Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa .

♦Kuna huzun ya kufanyiwa dhihaka kukataliwa kutoa maongozi na huku MUNGU amempa jukumu la kutuongoza katka hatua zoote za maisha yetu ya kila siku

πŸ“– Isaya 63:9-10 imeandikwa ‘Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, AKAWACHUKUA siku zote za kale. Lakini WAKAASI , wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao’.

Ukitazama hapa Kuna mambo utayaona lakn point yangu kubwa ipo kwenye eneo nlilotia wino mzito na kuendelea

πŸ“–Biblia inatuambia watu wake wakaasi na kwa sababu ya huo uasi Roho akahuzunika!

πŸ”₯ Na unaona MUNGU anakasirika na kuwa adui wao

♦ Moja ya gharama ya kumhuzunisha Roho Mtakatifu ni kwamba unajikuta upo kwenye wakat mbaya kwa sababu automatically unakuwa adui ya Mungu

πŸ’‘Sasa usikuchukulie mchezo Mungu akakuita adui yake 

Wakati ujao tutazam vitu vya mbele zaidi 

Neema ya Bwana Yesu ikufunike na kukupa amani ipitayo akili zote,,,